Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CAG abaini madudu CUF, CCM
Habari za SiasaTangulizi

CAG abaini madudu CUF, CCM

Charles Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
Spread the love

CHAMA cha Wananchi (CUF) na Chama Mapinduzi (CCM), vinatajwa kwa matumizi mabaya ya fedha katika Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali katika Mwaka wa Fedha 2018/19. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Charles Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ametoa kauli hiyo leo tarehe 26 Machi 2020 jijini Dodoma, wakati akimkabidhi Rais John Magufuli ripoti hiyo.

Kichere amesema, ukaguzi huo umebaini kwamba CUF ilihamisha fedha za ruzuku kiasi cha Sh. 300 milioni kati ya Sh. 366.38 milioni, kutoka kwenye akaunti yake ya benki kwenda katika akaunti binafsi ya mwanachama wa chama hicho, kinyume cha sheria.

Pia, amesema CUF haikuwasilisha nyaraka za matumizi za fedha hizo kwake, kwa ajili ya kuzifanyia ukaguzi.

“Ukaguzi wa vyama vya siasa, nilibaini CUF kilipokea ruzuku kutoka serikalini kiasi cha Mil. 366.38 lakini chama hicho kilihamisha mil 300 kutoka akaunti ya chama na kwenda katika akaunti binafsi ya mwanachama.

“Mil 66 zilitolewa kama fedha tasilimu, hata hivyo nyaraka za matumizi za fedha hizo hazikuwasilishwa kwangu kwa ajili ya ukaguzi. Pia, nilibaini mil 47 zilitolewa katika akaunti ya benki ya chama, pasipo idhini ya katibu mkuu wa chama, “ameeleza Kichere.

Pia ameeleza, CCM kupitia jumuiya yake ya wazazi ilifanya matumizi yasiyokuwa na tija kwa kumfidia mpangaji hasara ya kiasi cha Sh. 60 milioni, baada ya kukiuka masharti ya mkataba wa upangishaji.

“Matumizi yasiyokuwa na tija ya kumfidia mpangaji pasipo kufuata taratibu, kiasi cha Sh. mil 60 jumuiya ya wazazi ilitoa baada ya kumuondoa mpangaji bila kufuata utaratibu na mpangaji kuonesha nia ya kufungua kesi ya madai. Jumuiya hiyo ililazimika kulipa fidia ya hasara baada ya mazungumzo nje ya mhakama,” amesema Kichere.

Katika hatua nyingine, Kichere amesema katika ukaguzi wake, alibaini vyama vya siasa vinne vilipata hati isiyoridhisha na 11 vilipata hati mbaya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

error: Content is protected !!