Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rushwa CCM; Makada waanza kumimina fedha mtaani 
Habari za Siasa

Rushwa CCM; Makada waanza kumimina fedha mtaani 

Spread the love

MAKADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaosaka ubunge na udiwani kupitia chama hicho, wameanza kumimina fedha mtaani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa za makada hao kuanza kugonga wajumbe, imekuwa ikizungumzwa na Hamphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenenzi wa CCM ambapo sasa, Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais amewanyooshea kidole.

Taarifa ya CCM iliyotolewa leo tarehe 13 Februari 2020, wakati wa Maadhimisho ya Miaka 43 ya CCM, jijini Dar es Salaam, imeeleza orodha ya majina wanaotembeza mlungula ipo mikononi mwa viongozi wa juu.

Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais amewaeleza wajumbe kwenye maadhimisho hayo, kwamba vitendo hivyo vimeanza kushamiri.

“Nina fununu na nimepewa na majina kwamba, kuna watu wameanza kujipitisha mapema katika majimbo. Tayari kuna vijifedha vinatoka, kuna vijitakrima vinatolewa, lakini nataka niwaambie jicho la chama, jicho la serikali liko wazi tunawaona,” amesema na kuongeza:

“Na tayari tuna majina machache hapa, kama wewe ni mchezaji subiri filimbi ipigwe, halafu wote mcheze kwenye uwanja sawa, usianze kucheza kujisogeza golini, filimbi ikipigwa unatia tu golini, hiyo haiwezekani.”

Wakati huo huo, Mama Samia amewataka viongozi na wanachama wa CCM kutobweteka katika kutekeleza ujenzi wa chama hicho.

“Na hili nalo nataka nilisemee, tuna mtindo wa slogan hizi. Wataweza hawawezi, watatuweza aah wapi, lakini nataka niwaambie tusipofanya kazi tutawawezesha. Kutuweza hawatuwezi lakini tutawawezesha.

“Sasa niseme tudumu na itikadi zetu, tudumu na tunayoyasema. Tukisema wataweza aah wapi, iwe wapi kweli, tukisema hawezi wawe hawawezi kweli, sio tuseme mdomoni lakini mioyoni mwetu tofauti kweli,” amesema Mama Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari za Siasa

Wizara ya Kilimo yapanga kutumia Sh. 1.2 trilioni 2024/25

Spread the loveWIZARA ya Kilimo, imepanga kutumia bajeti ya Sh. 1.2 trilioni...

error: Content is protected !!