Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mlango ajira JKT wafunguliwa
Habari Mchanganyiko

Mlango ajira JKT wafunguliwa

Spread the love

MLANGO wa ajira umefunguliwa kwa vijana waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), na kufanya kazi ya kujitolea kwa miaka miwili. Anaripoti Dandon Kaijage, Dodoma … (endelea).

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeeleza, wahitimu wenye sifa wawasilishe taarifa zao binafsi (CV), vyeti vya elimu, taaluma na vyeti vya kuhitimu mafunzo ya JKT katika ofisi hiyo ili wapate kuajiriwa.

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 24 Desemba 2019 na Dk. Laurean Ndumbaro, Katibu Mkuu wa ofisi hiyo mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo jijini Dodoma.

Amesema, serikali katika juhudi za kuwajengea vijana uadilifu, umoja na mshikamano, inatarajia kuwapa ajira vijana waliohitimu mafunzo hayo.

Na kwamba, ajira hizo zitawahusu vijana wanaojitolea kwenye kambi mbalimbali za JKT, kwa muda wa miaka miwili tangu wahitimu mafunzo yao.

“Kwa kutambua mchango wa vijana ambao wamekuwa wakijitolea na hawajapata  ajira hadi sasa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli, ameelekeza vijana wote wenye shahada ya kwanza waliohudhuria na kuhitimu Operesheni Magufuli na waliojitolea wapewe ajira,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!