April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Askofu Shoo agonja kisu kwenye mfupa

Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dk. Frederick Shoo

Spread the love

TABIA ya utekaji, utesaji, unyongaji haki, dhuluma na kiburi inayolalamikiwa nchini, imekemewa vikali na Dk. Frederick Shoo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Anaripoti Mwandishi Wetu, Moshi … (endelea).

Akitoa salamu za Krismasi kwenye ibada iliyofanyika katika Kanisa la KKKT, Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro leo tarehe 25 Desemba 2019, Dk. Shoo amewataka watu waliojaa viburi vinavyojengwa na nafasi zao za uongozi, waache ili wawe salama mbele ya Mungu.

Kiongozi huyo wa dini amesema, watu waliompokea Yesu mioyo yao haina kiburi  wala majivuno. Amesema, kuna watu wanaotesa wenzao wasiokuwa na hatia jambo ambalo halimfurahishi Mungu.

“Yesu Kristo akatuguse mioyo yetu, tubadilike, tuache kiburi, tuache kuwatesa binadamu wenzetu na tuache kufurahia kuwatesa wenzetu wasio na hatia,” amesema Dk. Shoo.

Licha wateswaji kukumbana na matuio ya kikatili kutoka kwa wenye mamlaka, Dk. Shoo amewatia moyo kwamba, mateso yao hayapotei na kwamba ipo siku mateso ya watesaji yatafika ukomo wake.

“Katika kuteseka kwenu, kwa namna yoyote ile, hata tunapoteswa bila hatia, tujue kwamba Mungu yupo pamoja nasi, hivyo usiogope na usikate tamaa wala kuondoa tumaini lako kwa Mungu,  kwani mateso unayokutana nayo kwenye maisha, jua hakika yana mwisho wake,” amesema Dk. Shoo.

error: Content is protected !!