Saturday , 4 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mfumuko wa bei wapanda – Serikali
Habari Mchanganyiko

Mfumuko wa bei wapanda – Serikali

Dk. Ashatu Kijaji, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Spread the love

SERIKALI imeeleza kuwa mfumuko wa bei wa taifa, umeongezeka kwa asilimia 0.2 kutoka asilimia 3.4 Septemba hadi asilimia 3.6 Oktoba mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Dk. Ashatu Kijaji, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango leo tarehe 13 Novemba 2019, bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali lililohoji, mkakati wa serikali katika kudhibiti changamoto ya mfumuko wa bei katika bidhaa muhimu, hasa vyakula.

“Ni sahihi kabisa mfumuko wa bei wa taifa kwa mwaka ulioshia mwezi Oktoba mwaka 2019 umeongezeka hadi asilimia 3.6,  kutoka asilimia 3.4 kwa mwaka ulioshia mwezi Septemba 2019,” ameeleza Dk. Kijaji.

Dk. Kijaji amesema kilichopelekea mfumuko wa bei kuongezeka hasa katika bidhaa za vyakula aina ya unga wa mahindi na maharagwe, ni  baadhi ya maeneo hapa nchini kutopata chakula cha kutosha.

“Nna katika bidhaa zilizochangia ongezeko hili la asimia 0.2 ni bidhaa za chakula, kama taifa tunafahamu hatuna upungufu wa chakula. Tuna chakula cha kutosha, lakini yako maeneo ndani ya taifa letu ambayo hayakupata chakula cha kutosha, na hivyo yamepelekeea kuongeza bei ya bidhaa hizi,” amesema Dk. Kijaji.

Kufuatia changamopo hiyo, Dk. Kijaji amesema Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imeanza kutoa chakula kwa bei nafuu katika maeneo yenye upungufu wa chakula, ili kupunguza bei ya bidhaa hizo.

“Kama taifa tunalitambua hili, na tayari NRFA wameshatoa angalizo kutoa chakula hiki kwa wafanyabishara.

“Wanunue kwa bei nafuu ili kupeleka maeneo ambayo yana upungufu, na hatimaye kupunguza bei ya chakula na taifa letu ya kuwa na mfumuko wa bei mdogo na watanzania kupata chakula na bidhaa nyingine kwa bei rahisi na wanazozimudu,” amesema Dk. Kijaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!