Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waraka mpya vitambulisho ujasiriamali kutolewa
Habari za Siasa

Waraka mpya vitambulisho ujasiriamali kutolewa

Spread the love

SERIKALI imesema, ifikapo Julai Mosi mwaka huu itatoa waraka mahsusi utakaoainisha wajasiriamali wanaopaswa kupatiwa vitambulisho. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 25 Juni 2019 bungeni Jijini Dodoma na Mwita Waitara, Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wakati akijibu swali la Andrew Chenge, Mbunge wa Bariadi Magharibi, aliyeitaka serikali kutoa maelekezo ya utekelezwaji wa zoezi la ugawaji vitambulisho vya wajasiriamali nchini.

Akiuliza swali bungeni, Chenge amesema ni vyema serikali ikatoa maelekezo ya jinsi ya kutekeleza zoezi hilo ili liende kwa usawa katika maeneo yote nchini.

“Kwa kuwa vitambulisho vya wajasiriamali pamoja na nia njema iliyo nyuma yake,  utekelezaji wake bado ni kero nchini. Je serikal pia haiwezi ikatoa maelekezo ya jinsi ya kutekeleza zoezi hilo ili tuwe na usare nchi nzima kuliko hali ilivyosasa?” amehoji Chenge.

Akijibu swali hilo, Waitara amekiri uwepo wa changamoto katika utekelezaji wa zoezi hilo, na kusema kwamba kuanzia mwaka ujao wa fedha wa 2019/20 serikali itatoa waraka unaoanisha aina za wajasiriamali wanaopaswa kutozwa kodi na wale wanaotakiwa kupewa vitambulisho.

Amesema atakayekiuka maelekezo hayo, watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

“Pamoja na waraka wetu uliotolewa nchi nzima bado kuna changamoto ya utekelezaji wa zoezi hili. Tulisema tunapoanza Julai mosi tutatoa waraka mahsusi na wabunge mtapata nakala. Ukianisha nani anapaswa kutozwa kodi ya wajasiriamali na nani anapaswa kupewa kitambulisho,” amesema Waitara na kuongeza.

“Bbaada ya kutoa waraka huo, wale wote watakaokwenda kinyume na maelekzo hayo ambayo kimsingi sio matakwa ya serikali, sababu Rais John Magufuli alimaanisha kuwasaidia wajasiriamali wadogowadogo wasipate usumbufu kutozwa kodi kubwa, watachukuliwa hatua za kisheria.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!