Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Michezo Rais Magufuli awapa moyo Taifa Stars, akubali mziki wa Senegal
Michezo

Rais Magufuli awapa moyo Taifa Stars, akubali mziki wa Senegal

Spread the love

RAIS John Magufuli amewapa moyo wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kufuatia kupoteza mchezo wao wa kwanza katika Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 nchini Misri dhidi ya Segenal kwa mabao 2-0, kuwa walifungwa na timu bora. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo tarehe 25 Juni 2019, Rais Magufuli amemtuma Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam anayetarajiwa kuelekea Misri kushuhudia michuano hiyo, kuwafikishia salamu zake wachezaji hao ya kwamba wasikate tamaa.

Rais Magufuli amesema licha ya Taifa Stars kupigwa mabao 2-0 na Senegal, wamepata mwanzo mzuri kutokana na timu hiyo kusheheni wachezaji wa kimataifa na kuongoza kwa ubora barani Afrika.

“Na mimi nina uhakika hata huo mwanzo siyo mbaya sana, kufungwa tugoli tuwili tu, kwa timu ambayo inaongoza katika Afrika ambayo wachezaji wote wanacheza nje, mimi ninafikiri tuwape moyo,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amewataka wachezaji wa Taifa Stars kujituma katika michuano hiyo ili ipate matokeo mazuri yatakayowawezesha kusonga mbele, huku akiwataka Watanzania kuiombea timu yao ili ipate mafanikio.

“Ninakuruhusu nenda (Makonda) si umesema ukienda tutashinda? Basi nenda kwa sababu sisi sote tunataka kushinda, ukawaambie wachezaji wasikate tamaa. Kwenye mpira kuna kushinda, kushindwa na kutoka sare. Wao wakazane wakajitume zaidi na si tuendelee kuwaombea kwa sababu kushindwa kwao ni kushindwa kwetu,” amesema Rais Magufuli.

Taifa Stars itacheza mchezo wake wa pili wa Kundi C katika michuano hiyo siku ya Alhamisi ya tarehe 27 Juni mwaka huu, dhidi ya Kenya kabla ya kumaliza mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya Algeria tarehe 1 Julai, 2019.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Unamalizaje ligi kama hujabeti na Meridianbet?

Spread the love JUMAPILI ya leo tutashuhudia mitanange kibao ambayo itamalizika kuanzia...

Michezo

Uingereza, Hispania, Italia na Ufaransa kinawaka leo

Spread the loveLIGI mbalimbali barani ulaya kuendelea leo na michezokadhaa mikali itakwenda...

Michezo

Leo mkwanja upo Meridianbet, usipishane nao

Spread the love  Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Michezo

Anza wikendi yako na Meridianbet, upige mkwanja wa maana

Spread the love Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

error: Content is protected !!