Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bobi Wine aswekwa rumande
Habari Mchanganyiko

Bobi Wine aswekwa rumande

Bobi Wine
Spread the love

MBUNGE wa Kyadondo Mashariki nchini Uganda, Robert Kyagulanyi ‘Bobi Wine’ amewekwa rumande katika Kituo cha Polisi cha Naggalama, akituhumiwa kuandaa maandamano ya umma kinyume cha sheria. Inaripoti Mitandao ya Kijamii…(endelea).

Kwa mujibu wa mitandao ya kimataifa, Bobi Wine anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Uganda tangu tarehe 29 Aprili 2019, na kwamba hatima ya dhamana yake itajulikana tarehe 2 Mei 2019.

Ofisa wa Polisi nchini Uganda, Fred Ennanga amesema Bobi Wine anazuiwa na polisi na kwamba uchunguzi wa tuhuma zake unaendelea. Amesema Mwanasiasa huyo aliongoza maandamano hayo pasipo kuomba ruhusa kutoka kwa polisi.

Bobi Wine anasota rumande ikiwa ni siku chache baada ya kuwekwa kizuizini na Jeshi la Polisi nyumbani wake. Mwanasiasa huyo anatarajiwa kupelekwa katika gereza la Luzira mjini Kampala.

Mwanasiasa huyo mpinzani nchini Uganda anatuhumiwa kuongoza maandamano hayo ya kupinga kodi ya kutumia mitandao ya kijamii, mwaka jana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!