MBUNGE wa Kyadondo Mashariki nchini Uganda, Robert Kyagulanyi ‘Bobi Wine’ amewekwa rumande katika Kituo cha Polisi cha Naggalama, akituhumiwa kuandaa maandamano ya umma kinyume cha sheria. Inaripoti Mitandao ya Kijamii…(endelea).
Kwa mujibu wa mitandao ya kimataifa, Bobi Wine anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Uganda tangu tarehe 29 Aprili 2019, na kwamba hatima ya dhamana yake itajulikana tarehe 2 Mei 2019.
Ofisa wa Polisi nchini Uganda, Fred Ennanga amesema Bobi Wine anazuiwa na polisi na kwamba uchunguzi wa tuhuma zake unaendelea. Amesema Mwanasiasa huyo aliongoza maandamano hayo pasipo kuomba ruhusa kutoka kwa polisi.
Bobi Wine anasota rumande ikiwa ni siku chache baada ya kuwekwa kizuizini na Jeshi la Polisi nyumbani wake. Mwanasiasa huyo anatarajiwa kupelekwa katika gereza la Luzira mjini Kampala.
Mwanasiasa huyo mpinzani nchini Uganda anatuhumiwa kuongoza maandamano hayo ya kupinga kodi ya kutumia mitandao ya kijamii, mwaka jana.
Leave a comment