Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kampeni kumsaka Azory yaanza
Habari Mchanganyiko

Kampeni kumsaka Azory yaanza

Spread the love

LICHA ya Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kutaka watu kutomtafuta mwandishi wa Azory Gwanda aliyetoweka katika mazingira ya kutatanisha tangu 2017, wito huo umepuuzwa. Anaripoti Bupe Mwakiteleko … (endelea).

Baraza la Habari nchini Tanzania (MCT), limezindua kampeni ya mtandaoni ya kumsaka Azory, mwandishi wa habari wa kujitegegemea wa Kampuni ya Mwananchi Communications (MCL), aliyetoweka katika mazingira ya kutatanisha wilayani Kibiti, Pwani.

MCT imezindua ukurasa rasmi wa kukusanya saini pamoja na maoni ya wananchi ‘Petition’ wanaotaka vyombo vya ulinzi na usalama kumtafuta Azory aliyetoweka kusikojulikana tangu tarehe 21 Novemba 2017, hadi apatikane.

Kampeni hiyo imezinduliwa katika tovuti ya Avaaz inayoshughulika na harakati za uhamasishaji wa wananchi katika masuala mbalimbali kuanzia ngazi ya jamii, kitaifa na kimataifa, kwa minajili ya kuzitaka mamlaka husika kufanyia kazi madai yao.

Watu takribani 45 wameshasaini katika ukurasa huo, na kwamba dhumuni la saini hizo ni kuitaka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kushughulikia suala hilo.

Dk. Mwakyembe siku ya Jumanne wiki iliyopita, akizungumza bungeni wakati ahitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha ujao, alitaka kupuuzwa kwa watu wanaotaka ripoti kamili ya kupotea kwa Azory.

Kauli ya Dk. Mwakyembe ilipingwa vikali na baadhi ya Watanzania ikielezwa kukiuka utu na haki ya kila Mtazania kuhifadhiwa na kulindwa na taifa lake.

“Kwamba tuhalalishe kupotea ama kuuawa kwa watu kwa kisingizio cha kupotea au kuuawa kwa watu wengi, ni jambo la kustaajabisha.  Lakini uhai wa mtu mmoja ni muhimu sana leo na kesho na tukinyamza, watapotea wengi,” alisema Deodatus Balile, Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF).

Kajubi Mukajanga, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) alisema, “siyo kosa, kuhoji alipo Azory. Hii ni haki ya msingi kwa kila raia wa Jamhuri ya  Muungano.”

“tunajua, vyombo vya habari kuhusu kupiga kelele Azory hatuishii hapo. Tunatumia kama kioo chetu kulalamika kuhusu uhuru na usalama wa vyombo vya habari. Lakini tunatambua alikuwa baba wa familia ana mke na watoto, ndugu na jamaa watatushangaa sana watu wanaohusiana naye tukikaa kimya,” alisema Absalom Kibanda , Mwenyekiti Mstaafu wa TEF.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!