Tuesday , 30 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Laini za simu kuzimwa Desemba 31
Habari Mchanganyiko

Laini za simu kuzimwa Desemba 31

Spread the love

WATU ambao hawatasajili laini zao za simu kwa alama za vidole, hawatoweza kuzitumia baada ya tarehe 31 Desemba 2019. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Atashasta Nditiye, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ametoa kauli hiyo bungeni na kwamba, usajili wa laini za mitandao yote ya simu nchini, umepangwa kuanza tarehe 1 Mei 2019.

Amefafanua kwamba, baada ya kuanza kwa zoezi hilo, serikali itafanya mapitio yake mwezi Septemba ili kuona hatua iliyofikiwa, huku lengo la kuzima laini ambazo hazitakuwa zimesajiliwa likiwekwa kuwa tarehe ya mwisho wa mwaka huu.

“Zoezi la usajili litaanza tarehe Mosi Mei na tutafanya review (mapitio) mwezi wa tisa ili kuona ni watu wangapi wamekwishasajiliwa lakini mwisho kabisa itakuwa tarehe 31 Desemba mwaka huu,” amesema Nditiye.

Amesema kuwa, takwimu walizonazo kupitia Malaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ni kuwa, Watanzania walio na vitambulisho vya uraia wamefika milioni 16.

Nditiyealitoa ufafanuzi huo baada ya Felista Bura, Mbunge wa Viti Maalum (CCM) kutaka kujua kuhusu malalamiko ya wananchi wengi ambao hawajapata vitambulisho hivyo, huku wakiwa na wasiwasi kwamba inawezekana laini zao zikafungwa kutokana na kutopata vitambulisho vya taifa.

Akifafanua zaidi Nditiye amesema, kampuni zote za simu nchini zimeelezwa kuanza kufanya usajili huo kwa njia ya lama za vidole, ikiwa ni baada ya kujiridhisha na utambuzi wa mtu kupitia kitambulisho cha uraia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TMA yapongezwa kuimarisha ubora na usahihi wa taarifa za Hali ya Hewa

Spread the love  WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

7 wafa Ulanga, mbunge alia kutelekezwa na mawaziri, Tanroad

Spread the loveWatoto saba wamepoteza maisha na zaidi ya kaya 70 kukosa...

Habari Mchanganyiko

Bil 12.4 zimetumika ujenzi wa miradi wilaya ya Momba

Spread the love MKUU wa wilaya ya Momba mkoani Songwe Kennan Kihongosi...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

error: Content is protected !!