Saturday , 15 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mwakyembe ang’ang’aniwa kila kona
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mwakyembe ang’ang’aniwa kila kona

Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Spread the love

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ametakiwa kujizuia kutoa kauli za kejeli, dhidi ya watu wanaotafuta taarifa za mahali aliko, Azory Gwanda. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

“Alipofiwa na mkewe, alionekana akilia kwa uchungu sana. Mkewe alikuwa dhahabu. Alikuwa muhimu sana kwa familia yake. Ndivyo hivyo ilivyo kwa Azory kwa mke wake na watoto wake,” ameandika mmoja wa wahariri akirejea kauli ya Dk. Mwakyembe aliyoitoa jana bungeni, jana tarehe 23 Aprili.

Dk. Mwakyembe aliliambia Bunge, wakati wa kuhitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake, Dk. Mwakyembe alikemea watu wote wanaotaka kupewa taarifa mahali aliko Azory.

Aidha, wadau wengine wa habari, wamepinga kauli ya Dk. Mwakyembe na wengine wamemtaka kuomba radhi.

Azory alikuwa mwandishi wa habari wa kujitegemea anayefanyika shughuli zake katika eneo la Kibiti, mkoani Pwani. Amepotea katika mazingira ya kutatanisha tokea Novemba 2017.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga amesema, “siyo kosa, kuhoji alipo Azory. Hii ni haki ya msingi kwa kila raia wa Jamhuri ya  Muungano.”

Amesema, baraza lake litaendelea kufuatilia suala hilo  hadi pale hatma yake itakapofahamika.

Kajubi amesema, ili kufanikisha hilo, hivi karibuni watazindua wito wa maombi ya mtandaoni (Petition) kuhusu kadhia hiyo na kwamba, wadau wa habari na Watanzania watakaokuwa tayari kupiga kura ya kuhoji alipo Azory, watapiga kura hiyo.

“Badala ya kusikitika watu wanapopotea, anatumia kigezo cha wengine waliopotea kuhalalisha kupotea kwa Azory? Hapana. Hii siyo sahihi,” ameeleza Kajubi na kuongeza, “kila mtu ana haki ya kujua alipo Mtanzania mwenzake.”

Anasema, “majibu haya yakitolewa na watu makini na wasomi, yanazidi kushamirisha hayo mashaka kuwa Azory amechukuliwa na watu wanaofahamika. Walau akae kimya, sisi tutaendelea kumtafuta na kuhoji mahali alipo.”

Kajubi amesema, kauli hiyo haileti afya katika harakati kuenzi na kuimarisha uhuru wa wanahabari na vyombo vya habari nchini.

“Ni  kauli ya kushangaza na kushtua kwa sababu tatizo moja halitatuliwi au halifutwi na tatizo jingine. Ukweli ni kwamba, watu wamepotea sana Rufiji.  Lakini hiyo haimaanishi wengine waliopotea na ambao wanafahamika, wasitafutwe ama serikali isihojiwe,” ameeleza.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile, ameeleza kusikitishwa kwake na kauli hiyo ya Dk. Mwakyembe. Amesema, wadau wa habari wataendelea kuhoji kuhusu tukio hilo kwa kuwa kulinyamazia, hakuleti taswira nzuri kwa nchi.

 “Kwamba tuhalalishe kupotea ama kuuawa kwa watu kwa kisingizio cha kupotea au kuuawa kwa watu wengi, ni jambo la kustaajabisha.  Lakini uhai wa mtu mmoja ni muhimu sana leo na kesho na tukinyamza, watapotea wengi,” ameonya Balile.

Amesema, “huyu ni mwanahabari mwenzetu, tunataka kujua kama yuko hai, na si tabia au sifa nzuri kwa serikali kutumia ukumbi wa Bunge kukiri kwamba imeshindwa; kwa sababu serikali haishindwi.”

Mwenyekiti Mstaafu wa TEF, Absalom Kibanda amesema, kauli ya Dk. Mwakyembe si nzuri na kwamba, kitendo cha wanahabari kunyamazia suala hilo, “ni sawa na kuwafungulia mlango watu wasiojulikana kuendelea kufanya matukio hayo.”

Amesema, “tunajua, vyombo vya habari kuhusu kupiga kelele Azory hatuishii hapo. Tunatumia kama kioo chetu kulalamika kuhusu uhuru na usalama wa vyombo vya habari. Lakini tunatambua alikuwa baba wa familia ana mke na watoto, ndugu na jamaa watatushangaa sana watu wanaohusiana naye tukikaa kimya.”

 Amesema, “tukikaa kimya, tutafungua milango kwa watu wasiojulikana kuendelea kufanya hivyo kwa wanahabari weingine. Binafsi Mwakyembe amenishangaza na kwa bahati mbaya, hajui kuomba radhi. Angekuwa muungwana, angesema kauli hiyo aliteleza na kuomba radhi wanahabari, ni jambo la kusikitika ni jambo la bahati mbaya huyo ndio Dk. Mwakyembe.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Mataifa Afrika Mashariki yawasilisha bajeti 2024/2025 inayolenga kukuza uchumi

Spread the loveMataifa manne ya Afrika Mashariki jana Alhamisi yamewasilisha bungeni bajeti...

Habari za SiasaTangulizi

Gesi asilia, petroli kodi juu

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya marekebisho kwenye...

Habari za SiasaTangulizi

Bilioni 155.4 kugharamia kicheko cha wastaafu 2022-2030

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amesema jumla ya Sh...

error: Content is protected !!