Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Simba yatua Dar kwa mafungu
Michezo

Simba yatua Dar kwa mafungu

Spread the love

BAADA ya kupoteza mchezo wao wa pili mfululizo kwa kufungwa 5-0 na Al Ahaly ya Misri mwishoni mwa wiki, katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika hatua ya makundi, Timu ya Simba imerejea nchini kwa mafungu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea)

Kundi hilo la kwanza limewasili leo tarehe 4 februari 2019 mchana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl Nyerere wakiongozwa na mtendaji mkuu wa klabu hiyo Crescentus Magori na kocha Patrick Aussems ambapo walikwenda moja kwa moja kambini.

Meneja wa klabu hiyo Patrick Rweyemamu amesema sababu kubwa ya timu hiyo kurudi kwa mafungu kulitokana na mabadiliko ya muda wa mechi, kwa sababu hapo awali mechi ilipangwa kuchezwa saa 1 jioni lakini baadaye ikabadilishwa na kupelekwa saa 3 usiku.

“Tulitegemea baada ya mechi kumalizika watu warudi usiku ule ule ili wafike Dar es Salaam siku ya Jumapili na kama wote tulivyopata taarifa tulitegemea mechi ichezwe saa 1 ikaja kubadilishwa ikachezwa saa 3, kwa maana hiyo ratiba ya muda wa kuondoka ilibadilika”

“Kwa hiyo kuna baadhi ya watu wataondoka Jumapili ambao toka awali tiketi zao zilikuwa hazina matatizo na kuna baadhi ya wachezaji wengi wataondoka Jumatatu” alisema Rweyemamu.

Simba inatarajia kuwakabili tena Al Ahaly February 12, 2019 kwenye dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika hatua hiyo hiyo ya makundi kombe la klabu bingwa.

Baada ya kupoteza mchezo huyo Simba inaendelea kusalia na alama zake tatu na kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi D na huku wakiwa wamebakiwa na michezo mitatu.

 

 

 

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!