Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Lugha tatizo utafiti wa kilimo cha umwagiliaji
Habari Mchanganyiko

Lugha tatizo utafiti wa kilimo cha umwagiliaji

Spread the love

WATAFITI kutoka Vyuo vikuu mbalimbali nchini wametakiwa kutafsiri tafiti zinazofanyika kwa lugha nyepesi ili kuweza kutumika na kutatua matatizo yanayopatikana kwenye maeneo mbalimbali kila wakati ikiwemo changamoto ya matumizi ya maji kiholela katika kilimo cha umwagiliaji iliyopo kwa sasa. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali za maji, Praxeda Karugendo alisema hayo jana wakati akizindua kitabu cha mwongozo wa kutathmini ubora na afya ya mto kwa njia ya TARISS fupi kilichoandaliwa na bodi ya maji bonde la Rufiji chenye malengo ya kufuatilia ubora wa maji kwa kutumia wadudu ambao ni viumbe hai ili kuhimili uharibifu wa mazingira ya mto na maji kwa ujumla.

Karugendo alisema kuwa ikiwa tafiti zinazofanyika zikiendelea kutafsiriwa kama ilivyokuwa hii ya kufuatilia ubora wa maji itasaidia pia katika matumizi ya maji katika kilimo cha umwagiliaji ambayo yapo kiholela.

“kwa sasa mnatafsiri kwa lugha rahisi na zinatumika,  hivyo nimefurahi sana kwa kuwa tumepata mahali pakuanzia, uwe ni mwanzo wa kushawishi tafiti zingine ambazo bado hazijatumika ipasavyo ikiwemo eneo la umwagiliaji na matumizi ya maji lipo vibaya” alisema Karugendo.

Alisema, katika mabonde mengi ya umwagiliaji Tanzania maji yanaonekana hayatoshi kutokana na njia zinazotumika katika umwagiliaji kuwa zipo kiholela.

Aidha Karugendo alisema, Tanzania ina vyanzo vingi vya maji vyenye changamoto nyingi kwa aliipongeza Wizara ya maji na Umwagiliaji kwa sasa kuona umuhimu wa kubuni muundo wa kusimamia maji kutokana na sera ya maji.

Hivyo aliwataka viongozi wa Jumuiya za wamiaji maji kujiona kuwa wao bado ni watu muhimu katika kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa.

Naye Mwenyekiti wa Mradi wa Shahidi wa maji, Herbert Kashililah alisema, rasilimali za maji zinaanza kuwa ni tishio ingawa watanzania wanaona tunayo mengi sana kwani kiwango cha maji kimeonekana kupungua na kuwa chini ya 1700 hadi 1800.

Alisema kiwango hicho kikizidi chini ya 1700 tunaanza kuingia kwenye mfumo wa uhaba wa maji na kuanza kupigana kutafuta maji.

“tusifike huko kwa kuwa wakimbizi wa kimazingira, watu wanaokimbia kutokana na athari zinazotokana na uharibifu wa kimazingira ikiwemo maji na maji ndio itakuwa sehemu ambayo sisi tutagombana” alisema.

Kashililah alisema, Tanzania ya Viwanda haiwezi kuanza peke yake hivi hivi kama hawataanza kulima ambapo dhana ya TARISSfupi iliyozinduliwa leo itakuwa na changamoto sana wakati huo kama viwanda vikiwa vingi watu wakilima sana kwa viatilifu na kumwaga kwenye mito na hivyo vimelea vya vidudu hai havitaweza kuonekana kabisa.

Hivyo alisema, ni vema wakaanza kufikiria mbali kwa kujiandaa na matokeo hayo ambapo alisema usimamiaji wa rasilimali za maji sio wa Taasisi ya bonde la mto rufiji pekee ni wetu sote ambapo tushirikiane na kuziwezesha Jumuiya za watumiaji maji kuwa mbele katika kusimamia maji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!