Tuesday , 30 May 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Walimu wakana kumuua mwanafunzi
Elimu

Walimu wakana kumuua mwanafunzi

Spread the love

WALIMU wa Shule ya Msingi Kibeta, Respicius Mtaganzira na Herieth Gerald wanaotuhumiwa kumuua kwa kukusudia aliyekuwa mwanafunzi wa shule hiyo, Sperius Eradius, wamekana mashtaka yao. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mwalimu Mtaganzira anadaiwa kumsababishia kifo Sperius aliyekuwa anasoma darasa la tano, kwa kumpiga baada ya mwalimu Gerald ambaye ni mtuhumiwa wa pili katika kesi hiyo, kulalamika kwamba amepoteza mkoba wake wakati mwanafunzi huyo alipompokea mizigo yake alipoingia kazini.

hata hivyo baadaye mkoba wake ulionekana. tukio la mauaji ya mwanafunzi huyo lilisambaa kwa haraka kwenye vyombo vya habari na kuzua mjadala kwa wiki kadhaa mfululizo.

Washtakiwa hao leo tarehe 22 Oktoba 2018 walisomewa mashataka yao na hoja za awali na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Athuman Matuma katika Mahakama Kuu Kanda ya Kagera.

Kesi hiyo imehamishiwa Mahakama Kuu ikitokea Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba, baada ya upande wa jamhuri kukamilisha ushahidi ambapo leo ilisikilizwa kwa mara ya kwanza.

Mwalimu Mtaganzira na Gerald wameshtakiwa mahakamani hapo kwa kosa la mauaji ya kukusudia, walilodaiwa kutenda tarehe 27 Agosti mwaka huu kwenye maeneo ya shule ya msingi Kibeta.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

SUA kuhakikisha tafiti zinazofanywa zisiachwe kwenye makabati

Spread the love  MRATIBU wa utafiti na machapisho katika kurugenzi ya uzamiri,...

Elimu

Watakaopata Division One St Anne Marie Academy kupewa iphone ya macho matatu

Spread the loveMkurugenzi wa shule za St Anne Marie Academy, Dk. Jasson...

Elimu

Prof. Muhongo apinga TAMISEMI kusimamia elimu

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, ameshauri masuala...

Elimu

SUA kuboresha ufundishaji kupambania ajira za wahitimu

Spread the love  CHUO kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) mkoani hapa...

error: Content is protected !!