Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Giza nene latanda Chadema, wagombewa wake hofu tupu
Habari za SiasaTangulizi

Giza nene latanda Chadema, wagombewa wake hofu tupu

Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mch. Peter Msigwa
Spread the love

GIZA nene limetanda kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Iringa baada ya wagombea wake watatu wa udiwani katika uchaguzi mdogo kukutwa hali ya sintofahamu iliyowafanya kuingiwa na uoga wa kuwania nafasi zao katika uchaguzi huo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika wagombea hao watatu, mmoja ameporwa fomu ya kuwania nafasi hiyo, mwingine amekamatwa kwa madai ya kufoji fomu huku mwingine akitoweka pasipojulikana na baadaye kukutwa polisi na kuzuiliwa asizungumzke kitu chochote.

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amesema kwamba sintofahamu hiyo ilianza kujitokeza siku ya juzi baada ya aliyekuwa mgombea wa Kata ya Kwakilosa, Godfrey Luchagile kunyang’anywa fomu na mtu aliyemuonyesha bastola hali iliyomuingiza woga mgombea  na kumfanya ajitoe katika kinyang’anyiro hicho.

Msigwa amesema kwamba mgombea mwingine wa Kata ya Galilonga, Pallaiga Andrew yeye amekamatwa na jeshi la polisi kwa kosa la kugushi fomu ya uchaguzi akiwa eneo la kurudisha fomu yake.

Mbunge huyo amesema kuwa baada ya Luchagile kujitoa nafasi yake ilichukuliwa na Hamid Mfalingungi ambaye naye alipotea jana katika mazingira ya kutatanisha kabla ya kuonekana leo akiwa kituo cha polisi, lakini hakuzungumza chochote kutokana na kuzuia kufanya hivyo na jeshi la polisi.

Katibu wa Chadema Iringa, Jackson Mnyamwani amesema kuwa wakati sinema hiyo inaendelea Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, kata ya Kwakilosa, Fuad Mwakitosa amegoma kupokea fomu ya mgombea ambaye ilirudishwa na wadhamini wake kitu ambacho ni kinyume na utaratibu.

Pamoja na hayo, Mch Peter Msigwa amesema kwamba tayari siku ya jana walikwisha wasiliana na Mkurugenzi wa Uchaguzi Taifa, Athuman Kihamia kwa ajili ya sintofahamu hiyo lakini mpaka sasa hakuna kitu kinachoonekana kuendelea.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Juma Bwire hakupatikana kuzungumzia tukio hilo.

Uchaguzi wa marudio unatarajiwa kufanyika Agosti 12, 2018, katika jimbo la Buyungu, Kigoma na kata 77 baada ya madiwani wengi kuhama vyama vya upinzani na kuhamia CCM wakidai wanaunga mkono juhudi za Rais John Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!