Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Diwani, dereva wa Halmashauri Meatu wafariki ajalini
Habari za SiasaTangulizi

Diwani, dereva wa Halmashauri Meatu wafariki ajalini

Spread the love

DIWANI wa Kata ya Manuzi, Elias Shukia na dereva wa halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Haruna Ngata wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka mkoani Dodoma, kupasuka tairi na kupinduka mara tatu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa za awali kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu zinaelea kuwa ajali hiyo imetokea eneo la Mkiwa, Wilayani Singida.

Mtaturu amesema mkuregenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Fabian Manuzi; mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Piuz Machungwa na watu wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali hiyo.

Amesema majeruhi wanne wamelazwa katika hospitali ya St Gasper iliyopo Itigi na wawili wamelazwa hospitali ya Puma iliyopo wilayani Ikungi.

“Chanzo tulichokiona kwenye eneo la tukio ni kupasuka kwa tairi la mbele kushoto, hata hivyo tuwasubiri polisi wafanye uchunguzi zaidi watatuambia chanzo cha ajali yenyewe,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!