Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mil 160 zakatika kwenye uvuvi haramu
Habari Mchanganyiko

Mil 160 zakatika kwenye uvuvi haramu

Vyavu ambazo haziruhusiwi kuvulia zikiteketezwa kwa moto
Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum, Fakharia Shomari Khamis (CCM) ameihoji serikali namna ilivyojipanga katika kuzuia uvuvi haramu nchini, anaandika Dany Tibason.

Akiuliza swali bungeni leo, mbunge huyo pia ametaka kujua ni meli ngapi zilizokamatwa kwa sababu ya uvuvi haramu kuanzia mwaka 2010/15 lakini pia alitaka kujua ni watu wangapi wametiwa hatiani na hukumu zao zikoje.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha amesema katika kukabiliana na uvuvi haramu wizara imeanzisha na kuimarisha vituo 25 vya doria kwenye maziwa makubwa mwambao na Bahari ya Hindi na mipaka ya nchi.

Amesema vituo hivyo vipo katika maeneo ya Tanga, Dar es Salaam, Kigoma, Musoma, Kagera, Mwanza na Mtwara.

Vile vile amesema vituo vingine vipo Mafia, Kilwa, Horohoro, Kipili, Kasanga, Sota, Sitari, Kasumulo, Mbamba Bay Tunduma, Kanyigo, Rusumo, Ikola, Geita, Buhingu, Namanga na Murusagamba.

Amesema kuwepo kwa vituo hivyo kumeongeza uwezo wa kukabiliana na uvuvi na biashara haramu kupitia operesheni mbalimbali huku akisema kuwa pamoja na jitihada hizo za serikali tatizo la uvuvi haramu na biashara ya magendo kwenye mialo masoko na mipaka ya nchi bado ni kubwa.

Aidha amesema kuanzia mwaka 2011/15 jumla ya vyombo 2,795, injini za mitumbwi 118, magari 297 na pikipiki 33 vilikamatwa kwa sababu ya uvuvi haramu na utoroshwaji haramu kwenye maji hayo.

Amesema katika kipindi hicho jumla ya watuhumiwa 3,792 walikamatwa na kesi 243 zilifunguliwa mahakamani ambapo jumla ya Sh. 158,559,323 zilikusanywa ikiwa ni faini kutokana na makosa mbalimbali huku akisema katika kipindi hicho hakuna meli ya uvuvi iliyowahi kukamatwa.

Amewaomba wabunge ambao ni wajumbe katika halmashauri waendelee kutoa elimu kwa wavuvi kuhusu madhara ya uvuvi haramu na kuhimiza halmashauri zao kudhibiti uvuvi haramu kwenye maeneo yao.

Pia ameshauri jamii za wavuvi na wadau wote washirikishwe katika kusimamia rasilimali za uvuvi na matumizi endelevu kwa ajili ya kuwapatia wananchi ajira, chakula na u chumi wao na Taifa kwa ujumla kwa lengo la kudhibiti uvuvi haramu.

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!