Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Matajiri Dodoma watangaziwa vita
Habari za SiasaTangulizi

Matajiri Dodoma watangaziwa vita

Mji wa Dodoma
Spread the love

MKURUGENZI wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi amewatangazia vita matajiri wakubwa waliopora na kujilimbikizia viwanja bila kuviendeleza kwa wakati, anaandika Dany Tibason.

Kunambi amesema wale wote ambao wanamiliki viwanja vingi ndani ya manispaa bila kuviendeleza kwa mujibu wa sheria na taratibu wataporwa viwanja hivyo na kupewa watu wengine ambao wanauhitaji wa viwanja na kuviendeleza.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa akiwa katika ofisi iliyokuwa ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA, amesema tayari wamesaini hati ya makabidhiano baina ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma na iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) ambayo imevunjwa na Rais, Dk. John Magufuli hivi karibuni na kuelekeza shughuli zote kufanya na halmashauri ya Manispaa.

Aidha amesema kwa sasa wanatarajia kuunda kikosi kazi ambacho kitasimamia upitiwaji wa hati ambazo awali umiliki wake ulikuwa miaka 33 na kufikia miaka 99.

Mkurugenzi huyo, amesema pia wanatarajia kusaini mkataba wa hati ya makabidhiano ya jumla.

Amesema, wapo watu ambao wamejilimbikizia na kuhodhi viwanja kati ya 10-30 huku wakiacha bila kuviendeleza na wakijua kuwa sheria inasema usipoendeleza kiwanja cha makazi ndani ya miaka mitatu kwa mujibu wa sheria unapaswa kunyang’anywa.

Mkurugenzi huyo, amesema watu hao ni matajiri ambao wanaodai viwanja hivyo ili waweze kuviuza baadaye na kuwanyima fursa watanzania wengine ambao wanahitaji viwanja vya makazi.

“Katika hili najua nitakuwa nimemshika Simba sharubu kwa kuwa watu ni ninaoenda kushughulika nao ni matajiri na wanafedha, hivyo lolote linaweza tokea, lakini nimejipanga na nimejiandaa kupambana nao, na hili tutalifanya wakati tunabaditilisha hati ndio mambo yote hayo yatabainika,” amesema.

Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo amesema wameanza rasmi kutekeleza maagizo yaliyotolewa na rais ikiwa ni pamoja na kubadilisha hati kutoka miaka 33 ya sasa hadi kufikia miaka 99 ambayo ni kwa mujibu we sheria ya

Amesema katika kutekeleza jukumu hilo watashirikiana na wizara ya ardhi ambapo wataenda kikosi kazi kitakachoshiriki katika katika kazi yote ya kubadili hati hizo kazi ambayo itaanza mara moja kuanzia hivi sasa.

“Tunatarajia kazi hiyo haitachukua muda mrefu, kwanza kamishna wa ardhi tunataka kumtafutia chumba ndani ya ofisi hii ili kazi iweze kufanyika kwa urahisi kwa kikosi kazi chote kuwa sehemu moja,” amesema Kunambi.

Amesema mpaka mamlaka hiyo inavunjwa tayari ilishakabidhiwa hati 560,000 kwa wananchi ambazo zilichukua kipindi cha miaka 30 kuandaliwa, licha ya kuwa bado kuna watanzania ambao wanamiliki viwanja na bado hawajapatiwa ridhi.

Aliwatoa hofu wananchi ambao wanahofu kuvunjwa kwa CDA kutaleta madhara na kwamba wasihofu kwa chochote kilichobadilika ni jina na si kingine mana hiyo ni serikali hivyo majukumu yote yaliyokuwa yakifanywa na CDA yatafanywa na Manispaa kikamilifu na kwa kufuata Sheria.

Kunambi amesema kuondoka kwa CDA siyo msalia mtume kwa wake ambao wamejiunga holela sheria zitafanya kazi, waliojenga holela watabomolewa si kwa uonevu lakini haki itatendeka.

Aliwataka kutunza barua za toleo (ofa) na stakabadhi na kumbukumbu zote ili wanapoanza kufuatilia viwanja vyao wasipate shida maana hizo zitatumika kama ushahidi.

Mkurugenzi huyo amesisitiza, kuwa kuwa wataondoa urasimu ambao unapoteza malalamiko yote yaliyokuwemo awali.

Amesema baada ya kuvunjwa kwa mamlaka hiyo tayari kuna watu ambao wamekwisha anza kuvamia misitu na CDA ambapo aliwatahadharisha kuacha mchezo huo mara moja kwani mkono wa sheria utakuwa juu yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!