Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa 2 wasimamishwa DART kwa kugoma kusafirisha abiria
Habari za SiasaTangulizi

2 wasimamishwa DART kwa kugoma kusafirisha abiria

Spread the love

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umewasimamisha kazi watumishi wawili ambao ni Shabani Kajiru – Msimamizi wa Kituo cha Kivukoni na Brown Mlawa – Afisa Ufuatiliaji wa Kituo, ili kupisha uchunguzi kutokana vurugu  zilizotokea kati ya abiria na madereva wa basi la DART. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Vurugu hizo zilizotokea tarehe 26 Machi mwaka huu saa mbili usiku katika eneo la Kivukoni, zilitokana na abiria wengi waliokuwa wanasubiria basi la kwenda Kimara, kukaa kituoni kwa muda mrefu.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Mtendaji Mkuu wa DART, Athuman Kihamia leo Alhamisi umeeleza kuwa abiria hao waliamua kuingia kwenye basi la kuelekea Morocco lililokuwa kituoni hapo kupakia abiria wa Morroco na kumuamrisha dereva wa basi hilo akiwa na mwezake kuwapeleka Kimara.

Kihamia amesema madereva hao waliendelea kusimamia ratiba ya basi na kukataa kuwapeleka abiria hao Kimara na madereva hao kupeleka basi Morroco.

“Baada ya malumbano ya muda mrefu madereva wakaamua kuwarudisha abiria hao Kivukoni kitu ambacho sio busara,” amesema.

Amesema kwamba malumbano yalipozidi ndipo walipoamua kuwapeleka abiria hao Kimara.

“Wakala unamuelekeza Mtoa huduma wa Mpito (UDART) kuwachukulia hatua stahiki madereva Salehe Maziku na Chande Likotimo ambao walikua wanaendesha basi hilo kwa siku hiyo, msimamizi wa Kituo hicho, Lameck Kapufi pamoja na Afisa Usafirishaji, Erick Mukaro,” amesema.

Aidha, DART imetoa onyo kwa watumishi wake kuwa haitasita kuchukua hatua za haraka kwa watumishi watakaokiuka maadili ya utoaji wa huduma kwa wananchi wanaotumia usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka.

“Vilevile Wakala unaomba radhi kwa kilichotokea na unaahidi kuendelea kuboresha huduma zaidi kwa wananchi; Pia tuwatake wananchi wanaotumia usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka kufuata utaratibu uliowekwa na Wakala pamoja na mtoa huduma ya usafiri na wasisite kutoa taarifa pindi wanapoona kuna suala ambalo haliendani na utaratibu uliopo ili Wakala aweze kuchukua hatua za haraka,” imesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!