Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto ala kiapo mbele ya Wapemba
Habari za SiasaTangulizi

Zitto ala kiapo mbele ya Wapemba

Spread the love

ACT-WAZALENDO hakujapoa. Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na amsha amsha ya ‘ShushaTangaPandishaTanga Safari iendelee’ inavyotekelezwa visiwani Zanzibar. Anaripoti Bupe Mwakiteleko…(endelea).

Ni kauli mbiu iliyoasisiwa baada ya Maalim Seif Shariff Hamad, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF kujiunga na chama hicho ambapo baadhi ya viongozi na wanachama wa chama hicho wamemfuata.

Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo ni kama amepagawa baada ya maelfu ya waliokuwa wanachama wa CUF kutiririka kwenye mikutano inayoendelea Zanzibar kujiunga katika chama chake.

Akiwa Pemba kwenye mkutano wake na wakazi wa kisiwa hicho leo tarehe 23 Machi 2019 Zitto amekua ‘kiapo cha utii’ kwamba, chama hicho kitakuwa jukwaa madhubuti la kuendeleza mapambano ya kupigania haki zao.

Zitto amesema hayo alipozungumza na waliokuwa viongozi na wanachama wa CUF katika ukumbi wa Ngezi ulioko Chambani Mkoa wa Kusini Pemba.

“Kisiwa cha Pemba na wananchi wa Pemba mna historia kubwa katika mapambano ya kupigania haki, demokrasia na utu. Pemba imekuwa alama ya mapambano ya kupigania haki na demokrasia kabla na baada ya mfumo wa vyama vingi.

Mmekuwa walimu na mmetufundisha Watanzania maana ya kuwa na msimamo. Mmetufundisha maana ya ukweli katika kusimamia jambo mnaloliamini. Mmetufundisha maana ya kuwa utiifu kwa kiongozi mnayeamini anawakilisha na kusimamia kile mnachokiamini nyinyi,” amesema na kuongeza Zitto.

Zitto amesema kuwa, wakazi wa Pemba wana msimamo wa kweli na utiifu  kwa waliowaamini jambo ambalo litaendelea kuenziwa na ACT-Wazalendo.

“Kwa sababu ya msimamo, ukweli  na utiifu wenu kwa mnaloliamini na kulipigania, mmepitia katika hilaki na mateso makubwa sana.

“Pengine katika Tanzania hakuna eneo ambalo limeshuhudia hayo zaidi ya Pemba. Tunakuhakikishieni kuwa kujitoa kwenu si kwa bure na siku haiko mbali kile mlichokipigania mtakipata kupitia jukwaa hili la ACT,” amesema Zitto.

Amesema kuwa, Kisiwa cha Pemba na wananchi wake wana historia kubwa katika mapambano ya kupigania haki, demokrasia na utu na kuwa, wana alama ya mapambano ya kupigania haki na demokrasia kabla na baada ya mfumo wa vyama vingi.

“Kwa sababu ya msimamo, ukweli na utiifu wenu kwa mnaloliamini na kulipigania, mmepitia katika hilaki na mateso makubwa sana. Pengine katika Tanzania hakuna eneo ambalo limeshuhudia hayo zaidi ya Pemba.

“Tunakuhakikishieni kuwa kujitoa kwenu si kwa bure na siku haiko mbali kile mlichokipigania mtakipata Inshallah kupitia jukwaa hili la ACT,” amesema na kuongeza;

“Haya ni maumivu kwa jamii ya watu inayojitambua na kuwa na fakhari ya utu wao. Maisha kama haya yanatufanya tuwe dhalili na kuudhalilisha utu wetu. Pemba ni kisiwa chenye fursa nyingi na watu wabunifu tena wachapa kazi.

“Pemba inahitaji kufunguliwa kiuchumi kwa kuunganishwa na Unguja, Dar es Salaam, Tanga na Mombasa. Pemba inahitaji kuunganishwa na dunia kibiashara. Haya hayawezi kufanywa na CCM. Tunahitaji mabadiliko ili tupate Serikali inayothamini watu na kuziona fursa zilizopo Pemba na kuzifungua,” amesema Zitto.

Akizungumza kuhusu wanachama waliohamia ACT na kuchukua kadi kutoka Pemba, Zitto amewashukuru kwa hatua hiyo na kuwakaribisha ndani ya chama chake.

“Pemba ilikuwa ngome ya CUF chini ya uongozi wa Maalim Seif. Kwa hivyo, kitendo cha mliokuwa wanachama wa CUF nyote kwa umoja wenu kujiunga na jukwaa jipya la siasa la ACT Wazalendo kinaifanya Pemba sasa kuwa ngome ya ACT.

“Hili ni jambo kubwa sana kwa chama chetu. Tumewapokea kwa moyo mkunjufu na mjihisi mmefika na mko nyumbani ndani ya ACT. Karibuni sana!” amesema Zitto.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!