Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa BAVICHA si kikundi cha uasi – Sosopi
Habari za Siasa

BAVICHA si kikundi cha uasi – Sosopi

Spread the love

HIKI sio kikundi cha uasi. Hatutukani mtu hapa wala hatushauri vurugu. Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (BAVICHA) linafuata sheria na taratibu katika kufanya kazi zake. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Ni kauli ya Patrick Ole Sosopi, Mwenyekiti wa BAVICHA alipozungumza leo tarehe 23 Machi 2019 na MwanaHALISI ONLINE kutokana na tuhuma kuwa, baraza hilo limepoa tangu aingie madarakani.

Amesema, baraza lake haliamini katika siasa za fujo na matusi kwa kuwa si kikundi cha uasi na kwamba, kinafuata taratibu katika kutekeleza majukumu yake, ikiwemo kwa kuikosoa serikali kila unapokwenda kinyume.

“Sisi tunaongozwa na taasisi ya kisiasa, sio kikundi cha uasi. Tunafuata taratibu,  lengo ni  kuisukuma serikali na kueleza yale yasioenda sawa katika nchi Yetu. Kufanya fujo haitaonyesha kama baraza liko ‘active’,” Sosopi amesema na kuongeza;

“Unavyoongoza taasisi kubwa kama hii lazima tuwe na hulka ya kila namna, napenda kuwa na vijana wanaokosoa kistaarabu viongozi na si kutukana.

“Wakati mwingine tunajua vijana tuna mihemko. Tunataka chama kisiwe kinaamini katika fujo na ukiukwaji wa sheria, kazi yetu ni kuionesha serikali namna ya kufanya na kukosoa.”

 Hata hivyo ameeleza kukubali kuwepo kwa tuhuma kuhusu utendaji wa baraza analoliongoza. amefafanua kuwa, kuna tofauti kubwa ya kiutendaji kwenye baraza hilo kwa sasa kulinganisha na awamu za uongozi wa baraza hilo hapo awali.

Amesema, mabadiliko ya namna ya kuliendesha baraza hilo yamesukumwa kutokana na aina ya siasa zinazofanyika kwa sasa hapa nchini.

Amefafanua kuwa, zile kelele za BAVICHA zilizozoeleka kwa sasa hazipo akidai hali hiyo inatokana na upinzani kuzimwa kwa gharama kubwa kupitia Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

 “Kusikika kumepungua kutokana na aina ya siasa ilivyobadilika na namna ambavyo keleleza upinzani zinazimwa kwa gharama yoyote ikiwemo kupelekwa gerezani, lakini bado tunapaza sauti.

“Si sahihi kufafanisha baraza langu na la John Heche, sababu siasa za sasa na zamani ni tofauti. Sasa kuna siasa mpya,” amesema Sosopi.

Tazama video ya mahojiano hapo chini

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

Habari za SiasaTangulizi

‘Aliyemtonya’ Lissu kuhusu rushwa arejea madarakani

Spread the loveMwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Tutaendelea kupigania malengo ya afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Tanzania...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NHC yadai bil. 2.1 taasisi za Serikali, Waziri atoa maagizo

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii...

error: Content is protected !!