Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto: Akifika kwetu, anaonesha ubaguzi
Habari za Siasa

Zitto: Akifika kwetu, anaonesha ubaguzi

Spread the love

AKIFIKA kwenye majimbo yanaoongozwa na wapinzani, anasema “mmechelewa kwa sababu mlichagua wapinzani.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Mafia … (endelea).

Ni kauli ya Zitto Kabwe, kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni za ubunge kwenye Jimbo la Mafia tarehe 17 Septemba 2020.

Zitto ambaye  ni mgombea ubunge katika Jimbo la Kigoma Mjini na Saed Kubenea, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo na mgombea ubunge wa Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam, ni miongoni mwa wanasiasa wa chama hicho waliohudhuria uzinduzi huo na kumnadi Riziki Shahali Ngwali anayegombea ubunge katika jimbo hilo.

Saed Kubenea

“Mfano; kuna mgombea mmoja wa urais, kila sehemu kuna mbunge wa upinzani anasema, hapa hakuna maendeleo sababu mmechagua upinzani au akienda sehemu anasema, mkichagua wapinzani hautapata maendeleo,” amesema Zitto bila kumtaja jina mgombea huyo.

Amesema, hoja hiyo siyo kwa kweli kwa kuwa, hata katika maeneo yanayongozwa na wabunge na madiwani kutoka chama tawala, yanaongoza kwa kukosa maendeleo.

Akikazia hoja hiyo, Zitto ametolea mfano Jimbo la Mafia ambalo halijawahi kuongozwa na mbunge kutoka vyama vya upinzani, halina maendeleo.

Zitto Kabwe

Kufuatia changamoto hiyo, Zitto amewashauri Watanzania kuchagua wagombea wa upinzani ili wapate mabadiliko ya uongozi yatakayochochea maendeleo.

“Changamoto kubwa Mafia haiendelei ni sababu mmeikumbatia CCM, toka mfumo wa vyama vingi umeanza hamjawahi kupata mbunge kutoka upinzani,  hamjawahi kupatachangamoto mpya. Wabunge wenu walewale,” amesema Zitto.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!