Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Watoto wa Loliondo walazimika kuajiriwa kuyakabili maisha
Habari Mchanganyiko

Watoto wa Loliondo walazimika kuajiriwa kuyakabili maisha

Ngirimba Taineni akizungumza na waandishi wa habari
Spread the love

BAADA ya kuathirika kiuchumi kutokana na operesheni ondoa mifugo, katika vijiji vinavyopatakana na hifadhi ya Serengeti, Loliondo, wilayani Ngorongoro, sasa watoto walazimika kufanya vibarua vya kuchunga kwa ujira wa sh. 40,000 kwa mwezi, anaandika Nasra Abdallah.

Hayo yamebainishwa na mmoja wa wakazi wa kijiji cha Ololosokwani, Ngirimba Taineni alipokuwa akieleza athari zilizompata baada ya operesheni hiyo.

Taineni ambaye awali alikuwa akimiliki ng’ombe 220 ambao walikuwa wakimsaidia kuihudumia familia yake yenye watoto 23 na wake watatu, lakini baada ya mifugo hiyo kukamatwa ameshindwa kumudu mahitaji yao ya kila siku.

“Hivi sasa nalazimika kuwaruhusu watoto wangu wanapotoka shule kwenda kuchunga ili hela watakayopata isaidie kuhudumia familia kwani nguvu ya kuiangalia mwenyewe kwa sasa sina japo naumia kwa kuwa muda huo wangetakiwa wawe wanajisomea lakini sina namna, amesema mkazi huyo.

Amebainisha kwamba katika familia yake wanaoenda kuchunga ni watoto wake wanne ambao kila mwisho wa mwezi ana uhakika wa kupata Sh. 160,000 akichanganya na yeye ambaye hulipwa 100,000 kwa kuwa malipo huendana na umri wa mtu yanasaidia maisha kwenda.

Naye Wilson Kilonga, amesema kutokana na maisha yalivyo magumu kuna hatari ya wanaume kuwakimbia wake zao na kumuomba Rais John Magufuli kuangalia namna gani wanaweza kufidiwa mifugo yao ili warudi katika maisha yao waliokuwa wakiishi huko nyuma.

Kilonga amesema kwa yeye mpaka sasa ameshateketeza kiasi cha Sh. 700 milioni kwa ajili ya kulipa faini wakati operesheni hiyo inaanza na baadaye mifugo hiyo tena kukamatwa wakati wanakwenda kunywa maji eneo lililoruhusiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla alipositisha operesheni hiyo.

Kwa upande wake Mosiwa Dokwanyi amesema bei ya gunia la mahindi imependa kutoka Sh. 60,000 hadi 84,000 kiasi ambacho ni kikubwa kwao kutokana na hali ya maisha waliyonayo kwa sasa.

“Hali hii kwa kweli inatufanya tule mlo mmoja badala ya mitatu ukizingatia kwamba huko nyuma chakula chetu kikuu kilikuwa maziwa na sasa imetubidi tule ugali na kunywa uji kwa kuwa hatuna mifugo tena,” amesema Dokwanyi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!