Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanywaji pombe za kienyeji waonywa
Habari Mchanganyiko

Wanywaji pombe za kienyeji waonywa

Spread the love

DIWANI wa kata ya Ipagala jijini Dodoma, Doto Gombo, amewaonya wanywaji wa pombe za kienyeji kuacha tabia ya kuchangia chombo kimoja maarufu kwa jina la Chitochi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Diwani huyo alisema kuwa wanywaji wengi wa pombe za kienyeji wanatabia ya kuchangia chombo kimoja zaidi ya watanohadi kumi jambo ambalo ni hatarikwa afya zao.

“Nipende kusema kuwa marufuku hiyo si kwa wanywaji wa pombe ya kienyeji tu hata wavuta sigara wanatabia ya kugongeana jambo ambalo kimsingi ni baya na linaweza kuchangia maambukizi ya Virusi vya Corona,” alisema Gombo.

Kuhusu wauzaji wa pombe majumbani alisema kuwa wanatakiwa kuzingatia usafi na taratibu zinazotakiwa ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa, maji tililika na sabuni pamoja na vitakasa mikono.

Katika hatua nyingine alisema wanywaji wa pombe hizo wanatakiwa kujiepusha na msongamano usiokuwa wa lazima.

“Kutokana na hali ilivyo kwa sasa mtumiaji wa pombe za kienyeji anatakiwa kutumia chombo chake na siyo kuchangiana,” alisema Diwani.

Gombo ametoa tahadhali hiyo alipokuwa akitoa maelekezo kwa watendaji, wenyeviti na mabalozi wa mitaa kuhakikisha vilabu vya pombe za kienyeji na wanaouzia majumbani wanachukua tahadhali kuepukana na maambukizi ya ugonjwa huo ikiwemo na wao wenyewe.

Alisema katika kipindi hiki cha ugonjwa kila maeneo yanatakiwa kuchukuliwa tahadhali kubwa ya kujilinda na hakuna sababu ya kubembelezana ikiwemo huko kwenye vilabu vya pombe za kienyeji.

Alisema wenye vilabu hivyo wanatakiwa kuhakikisha wanakuwa na vyombo safi vinavyotumika kunywea na vinakuwa vingi na siyo vya kupokezana kwa kila mnywaji na wakifanya hivyo wanaweza kuwa chanzo kuenea kwa gonjwa hilo hatari.

“Niwatake sasa hao wenye vilabu vya pombe na wale wanaouzia majumbani,wahakikishe wanakuwa na vyombo vya kutosha, na maeneo yao kuna vifaa vya kujilinda kama vile barakoa,maji na sabauni na vitakasa mikono,” alisema.

Diwani huyo hata hivyo amewataka wakazi wa kata hiyo kila kaya kunakuwa na vifaa vya kujilinda wao wenyewe ikiwemo madumu ya maji na sabani, vitakasa mikono na barakoa.

Alisema kutokana na kuwepokwaugonjwa wa Corona hakuna sababu ya kuoneana aibu bali kila kaya inatakiwa kutekeleza maagizo yanayotolewa na wataalamu wa Afya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!