Saturday , 2 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Kaya 80 Dodoma zapokea msaada wa Mil 21
Habari Mchanganyiko

Kaya 80 Dodoma zapokea msaada wa Mil 21

Spread the love

JUMLA ya kaya 80 za wakazi wa Kata ya Chamwino Jijini Dodoma wamenufaika na msaada wa chakula na mahitaji mbalimbali kutoka, taasisi ya Dar-Ul-Muslimeen kwa kushirikiana na W.I.P.A.H.S. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Msaada huo wa chakula na mahitaji mbalimbali wenye thamani ya sh. 21 milioni utawalenga waumini wa dini ya Kiislam ambao wanatoka kaya zenye mahitaji maalumu ili ziweze kujikimu wakati wa kipindi cha Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Vijana na Watu wenye Ulemavu, Athony Mavunde, akipokea msaada huo  ameziomba taasisi za dini, mashirika ya umma na watu binafsi kusaidia watu wenye mahitaji maalumu hususani katika kipindi ambacho kuna janga la virusi vya ugonjwa wa corona.

Aidha kutokana na mlipuko wa virusi vya coron nchini, amewaomba wadau mbalimbali kuwasaidia waumini wasiojiweza wa dini ya kiislamu misaada ya vyakula vitakavyo wawezesha kutimiza moja ya nguzo ya dini hiyo.

Ushauri huo ametoa baada ya kupokea misaada ya chakula wenye thamani ya million 21 uliotolewa na taasisi hizo kwa waumini wa msikiti wa Hudda Chamwino jijini Dodoma.

Mavunde alisema kuwa katika kipindi hiki cha janga la ugonjwa wa corona kuna makundi mengi yanahitaji kusaidiwa mahitaji maalumu ikiwemo vifaa vya kujikinga na gonjwa hili.

Naibu Waziri huyo alisema kuwa ni wakati wa kutoa misaada ya vyakula kwa waumini wa dini ya kiislamu wanapoendea mwezi mtukufu ramadhani,ili waweze kujimudu kwa mguzo muhimu ya Uislamu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Dar-Ul-Muslimeen, Shekhe Muslim Bhanji, alisema kuwa jumla ya mifuko 300 ikiwemo mchele, maharange, sukari imetolewa kwa ajili ya kuwasaidia waumini wenye mahitaji maalumu wa msikiti wa Hudda wa Chamwino.

Pamoja na kusaidia kujikimu kwa Mwezi Mtukufu waumini waliopata msaada huo hawataweza kutembea  kutafuta mahitaji ikiwa ni pamojana kujikinga na maambukizi ya coroma.

Naye kwa upande wake Diwani wa kata hiyo ya Chamwino, Jumanne Gende (CCM) aliwataka waumini waliokabidhiwa misaada hiyo kuitumia kwa malengo yaliyokusudiwa  kutoka kwa wahisani hao.

Juma Kemo, Shekhe wa msikiti huo wa Hudda Chamwino akishukuru kwa kupatiwa msaada huo kwa niaba ya walengwa aliwataka kuuthamini huku pia wakijilinda na janga la maambukizi ya ugonjwa wa corona kwa kufuata maelekezo ya waatalamu wa afya na viongozi wa serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mwalimu jela miaka mitatu kwa rushwa

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu...

Habari Mchanganyiko

Waziri Bashungwa aagiza wahandisi kujengewa uwezo

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Bodi ya Usajili wa...

Habari Mchanganyiko

Heche ataka mawakili vijana kuamka sakata Mpoki

Spread the loveMWENYEKITI wa Mawakili Vijana Tanzania kutoka Chama cha Mawakili wa...

error: Content is protected !!