Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wanasiasa wanaodhalilisha wanawake wawajibishwe
Habari za Siasa

Wanasiasa wanaodhalilisha wanawake wawajibishwe

Spread the love

WANAMTANDAO wa Katiba, Uchaguzi na Uongozi ambao ni watetezi wa haki za wanawake na wasichana, wamelaani kauli za udhalilishaji zilizoanza kutolewa na baadhi ya wanasiasa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pia, wamezitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Msajili wa Vyama Vya Siasa na taasisi nyingine husika kuwachukulia hatua kali wagombea, pamoja na wapambe wao, wanaotoa lugha hizo zinazokatisha tamaa wanawake kushiriki kwenye chaguzi.

Wanamtandao wametoa kauli hiyo leo Alhamisi tarehe 3 Septemba 2020 baada ya kusambaa kwa video fupi mtandaoni ikimwonyesha mwanachama wa Chama Cha Mapindiuzi (CCM) Mkoa wa Mara akitumia lugha ya udhalilishaji kwa wanawake.

Mwanachama huyo alitoa lugha hiyo akiwaita wanawake wanaogombea ni ‘malaya’ katika mkutano wa kampeni alipokuwa akimnadi mgombea ubunge wa Tarime Mjini, Mwita Kembaki wa CCM.

Katika taarifa hiyo ya wanamtamndao wa masuala ya kukuza ushiriki wa wanawake  katika uongozi wa kisiasa wamesema, wamekuwa wakifuatilia  kwa ukaribu mkubwa mchakato mzima wa uchaguzi tangu ulipoanza.

Pia, wamefuatilia matukio mbalimbali ambayo tayari yameshajitokeza ikiwemo utumiaji wa lugha za matusi na kauli mbaya za udhalilishaji dhidi ya wanawake wanaogombea na wafuasi wa vyama kwa ujumla.

Wanamtandao hao wamesema, kitendo cha kutoa lugha za udhalilishaji  inarudisha nyuma jitihada za Serikali katika kufikia usawa wa kijinsia na kurudisha nyuma ari ya wanawake wengi kugombea nafasi za uongozi kwa sababu ya kuogopa kudhalilishwa.

“Halikadhalika, inanyamazisha sauti za wanawake ambao ni zaidi ya nusu ya Watanzania wote ambao ni wapiga kura wakuu na ambao wanahaki ya ushiriki salama katika masuala ya kisiasa, suala ambalo halina tija kwa taifa letu.”

“Kutokana na hali hii, tunaona umuhimu wa vyombo na mamlaka zinavyohusika kuwawajibisha kwa mujibu wa sheria, kanuni na maadili ya uchaguzi kwa wote wanaotumia matusi na lugha za kudhalilisha wanawake,” wammesema wanamtandao hao.

Katika hilo wamesema “tunaomba umma wa Watanzania na vyombo mbalimbali vinavyosimamia uchaguzi wa taifa hili utambua, ushiriki wa wanawake katika michakato ya uchaguzi ni haki yao ya kikatiba na zimebainishwa katika sheria mbalimbali za nchi.”

Wanamtandao hao wamewataka “viongozi wa taasisi mbalimbali zikiwemo za dini na hasa vyama vya siasa, Asasi za Kiaraia na jamii yote kwa ujumla ya Tanzania kukemea vikali tabia hizi za kudhalilisha wanawake hasa kipindi hiki cha uchaguzi.”

“Vyama vya siasa vitambue vina wajibu wa kulinda, kutetea na kudumisha haki na usawa wa wanawake ndani ya vyama vyao na katika jamii kwa ujumla, kwa kuwa wanawake ndiyo kundi kubwa la wapiga kura Tanzania.”

“Kwahiyo lazima viheshimu utu wa mwanamke na kutoa fursa na kuweka mazingira yaliyo ya wazi na wezeshi ili wanawake wengi washiriki kikamilifu katika kutimiza haki yao ya kikatiba kama wagombea  na wapiga kura,” wamesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!