Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Waliyoomba viwanja CDA kuponyeka
Habari Mchanganyiko

Waliyoomba viwanja CDA kuponyeka

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania
Spread the love

SERIKALI imesema kuwa kila mwananchi aliyeomba  kiwanja kwa iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) kuwa kiwanja chake hakitapotea baada ya mamlaka hiyo kuvunjwa, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo ilitolewa leo bungeni na Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu alipokuwa akijibu swali la Matha Mlata, Mbunge wa Viti Maalum (CCM).

Katika swali lake, Matha alitaka kujua nini hatma ya wananchi walionunua viwanja na hawajakabidhiwa na CDA na kwa sasa imevunjwa.

Waziri Mjaliwa amesema kwa sasa shughuli zote za CDA zimehamishiwa kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma na akaunti zake zote zimefungwa na ukaguzi wa kina unaendelea kujua kuna kiasi gani na matumizi yake.

Amesema mara baada ya kukamilika kwa ukaguzi huo shughuli zitarejea kama kawaida lakini zitafanywa na halmashauri ya Manispaa ya Dodoma na  huduma katika jengo lilokuwa la CDA zitaendelea na hapo hapo kutakuwa na Idara ya Ardhi.

“Tunataka mtu akiingia katika jengo hilo anaomba kiwanja na wakati huo huo anapata hati yake na jengo lile tunataka liandikwe ‘CDA idara ya ardhi’,’’ amesema.

Amesema kutokana na baadhi ya watumishi walikuwa wakilalamikiwa sana na wananchi hivyo watumishi hao watawekwa kando kabla ya kuhamishiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma na kuzitaka halmashauri zote nchini kuzingatia sheria pale wanapotwaa maeneo ya wananchi kwa kulipa fidia.

Aidha amesema ni lazima fidia ilipwe kwanza kabla ya kutwaa maeneo hayo na ilingane na thamani ya eneo husika.

‘’Zipo Sheria zonzoongoza katika masuala ya fidia na maeneo yote ni lazima yalipie fidia kwanza kabla ya kuyatwaa kwani wengine wanaweza kuwa na mazao katika maeneo hayo’’ amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!