August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Trump atoa masharti mapya Sudan, Somalia

Spread the love

UTAWALA ¬†wa Rais Donald Trump wa Marekani umeweka masharti mapya ya maombi ya kibali ‘Visa’ kutoka kwa mataifa sita ya Kiislamu pamoja na wakimbizi wote.

Masharti hayo ambayo yanawataka kuwa na mtu wanaohusiana ama ushirikiano wa kibiashara na Marekani inayoyahusisha mataifa yaliyo na Waislamu kama vile Iran, Libya, Somalia, Sudan , Syria na Yemen imeangaziwa katika ujumbe uliotumwa katika balozi zote.

Masharti hayo mapya yaliyoanza kufanya kazi siku ya leo yanaelezea mahusiano ya kifamilia kama mzazi, mkeo ama mumeo, mtoto wa kiume ama wa kike.

Masharti hayo ni baada ya Mahakama Kuu nchini Marekani kuidhinisha kwa muda agizo la Rais Trump ambalo lilikosolewa kuwa marufuku kwa Waislamu.

error: Content is protected !!