Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Ununuzi wa madiwani wahamia kwa Sugu,’ Dk. Tulia atajwa
Habari za SiasaTangulizi

‘Ununuzi wa madiwani wahamia kwa Sugu,’ Dk. Tulia atajwa

Joseph Mbilinyi 'Sugu,' Mgombea ubunge wa Mbeya Mjini. Picha ndogo, mshindi wa jimbo hilo, Dk. Tulia Akson
Spread the love

WIMBI la baadhi ya madiwani kukihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), linatarajiwa kuendelea kutikisa jiji la Mbeya. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Taatifa kutoka baadhi ya watu waliokaribu na Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Mbeya zinasema, tayari madiwani wengine wanne wako mbioni kuondoka Chadema na kujiunga na chama hicho.

MwanaHALISI Online limeshindwa kupata kwa uhakika, majina ya madiwani ambao wako kwenye mazungumzo ya mwisho ya kuondoka Chadema.

Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja siku tatu baada ya uongozi wa Chadema kwenye wilaya ya Mbeya Mjini, kutangaza kuwavua uwanachama madiwani watatu wake wa tatu.

Aidha, kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja katika kipindi ambacho mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameonya kuwa wanaodhani Mbeya Mjini ni “fursa ya ajira wanajidanganya na wanapoteza fedha zao.”

Sugu alitoa kauli hiyo katika mahojiano yake maalumu na gazeti la Mwananchi, Jumamosi iliyopita, tarehe 21 Julai 2018.

Alisema, “Mbeya Mjini ni sehemu tofauti sana. Napenda kuwashauri watu wengi ambao wanadhani kwamba Mbeya Mjini ni fursa ya ajira, haiko hivyo. Pale tuna majukumu ya kufanya, majukumu ambayo hayakufanywa toka uhuru mpaka tulipoingia kama Chadema kama Sugu mwaka 2010, mpaka sasa watu wanaona tofauti kilichofanyika tangu 2010 mpaka sasa.”

Kiongozi mmoja wa Chadema mkoani Mbeya amethibitisha kuwapo kwa mkakati wa kuwashawishi baadhi ya madiwani wa jiji la Mbeya kujiuzulu, ili kumdhoofisha mbunge wa jimbo hilo, Joseph Mbilinyi (Sugu).

Amesema, “Ni kweli kuwa kuna madiwani watatoka Chadema na kujiunga na CCM jijini Mbeya kutokana na madai ya kutofurahishwa na hatua ambazo zimechukuliwa kwa wenzao waliofukuzwa.”

Amesema, “hawa madiwani wanaotaka kuhama, wanadai kuwa katiba ya Chadema haitoi mamlaka kwa chama ngazi ya wilaya kufukuza madiwani. Kwa mujibu wake, kazi hiyo inapaswa kufanywa na Kamati Kuu (CC).”

Hata hivyo, kiongozi huyo ambaye anaonekana kuwa ndiye “wakala mkuu” wa CCM katika “kufikia ununuzi wa madiwani wa Mbeya Mjini,” hakueleza iwapo ni makosa kwa wilaya kuchukua hatua hizo ili kukinusuru chama chao.

Badala yake, anaishia kusema, “Katiba iko wazi, kwamba mamlaka ya nidhamu ya madiwani ni kamati kuu. Hivyo chochote ambacho kimefanywa na wilaya au mkoa, ni kinyume na katiba.”

Vuguvugu la kuondoka kwa madiwani wa Chadema katika halmashauri ya jiji la Mbeya, limepamba moto kufuatia kuwapo kwa madai kuwa baadhi ya madiwani wanampigia “chapuo,” Dk. Tulia Ackson Mwansasu, naibu Spika wa Bunge la Jamhuri.

Wanadai kuwa Dk. Tulia, anastahili kuwa mgombea ubunge na ana sifa ya kuwa mbunge wa Mbeya Mjini kuchukua nafasi ya Sugu mwaka 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!