February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Siku ya Mashujaa, JWTZ kufanya shughuli za kijamii

Msemaji Mkuu wa JWTZ, Kanali Ramadhani Dogoli

Spread the love

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kesho litaadhimisha Siku ya Mashujaa waliopoteza uhai wakipigania Taifa, kwa kufanya shughuli za mbalimbali za kijamii. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Msemaji Mkuu wa JWTZ, Kanali Ramadhani Dogoli amesema katika kuadhimisha siku hiyo, watatoa huduma ya vipimo vya shinikizo la damu, kisukari, uchunguzi wa kinywa na meno, ushauri nasaha na kupima VVU kwa hiari pamoja na kufanya usafi viwanja vya Mnazi Mmoja ambavyo vitatumika kufanyia vipimo hivyo.

Aidha, amesema Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu vitashiriki usafi katika maeneo mbalimbali yakiwemo Hospitali ya Temeke, Zakhiem, Dar Group na masoko ya Mbagala, Temeke, Tandika.

Pia amesema vikosi hivyo vitafanya shughuli za upandaji miti katika shule ya Wailes na stendi ya mabasi ya Mbagala na Temeke.

Kwa upande wa Zanzibar, Brigedia ya Nyuko watashiriki usafi katika masoko ya Mombasa, Sebuleni, Majumba ya Wazee na Mwanakwerekwe.

Shughuli zote zitatembelewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo.

error: Content is protected !!