Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko UNICEF: Cheti cha kuzaliwa ni ulinzi kwa mtoto
Habari Mchanganyiko

UNICEF: Cheti cha kuzaliwa ni ulinzi kwa mtoto

Spread the love

MKUU wa Kitengo cha ulinzi wa Mtoto kutoka UNICEF, Maud  Droogleever Fortuyn amesema kuwa usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano ni kinga Muhimu kwa ulinzi wa watoto kwa maisha yao ya baadaye. Anaripoti Danson Kaijage, Singida … (endelea).

Alisema mtoto ambayo hana cheti cha kuzaliwa anaweza kukosa huduma muhimu anazotakiwa kuzipata kwani utambulisho wake unakuwa mgumu kufahamika.

Mkuu huyo wa kitengo aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa usajili na ugawaji wa vyeti vya kuzaliwa watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano katika mkoa wa Singida na Dodoma na uzinduzi huo ulifanyika Mkoani Singida kwenye viwanja vya stendi ya zamani ya Majengo.

Alisema kuwa ili uweze kupata huduma nzuri ni lazima uwe umepata cheti cha kuzaliwa ambapo unaweza kupata huduma yoyote bila usumbufu.

Mbali na hilo Shirika la kuhudumia watoto duniani (UNICEF) ambalo ni mdau wa maendeleo limesema kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania wataakikisha wanawezesha uhamasishaji wa usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa nchi nzima.

Mkuu huyo wa kitengo alisema kuwa uhamasishaji huo utawawezesha wazazi kote nchini kuona muhimu wa kuwapatia vyeti vya kuzaliwa watoto ikiwa ni sehemu ya kuwatengenezea mazingira bora ya watoto hao kuingia katika mfumo rasmi wa kupata huduma bora na muhimu.

Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Augustine Mahiga akizungumza na wananchi na viongozi Mbalimbali  katika uzinduzi huo alisema kuwa licha ya kuwa wanasajili na kutoa vyeti lakini ni lazima kutunza kumbukumbu.

Mahiga alisema ili kuwa na maendeleo ya nchi ni lazima kuwa na takwimu sahihi za watu ulionao na ndiyo sababu ambao serikali iliiona na kuanzisha mpango huo.

Naye mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi alisema kuwa hatakuwa tayari kuona wanajitokeza watu ambao wanamakusudi ya kukwamisha mpango Usajili na uandikishaji wa watoto wenye umri wa miaka mitano.

Dk. Nchimbi alitoa angalizo hilo jana muda mfupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Katiba na Sheria Augustine Mahiga wakati wa uzinduzi wa mpango wa kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri wa miaka mitano.

Mpango huo wa uzinduzi wa kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano unaoendeshwa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana wadau wa maendeleo ikiwa ni pamoja na shirika la kuhudumia watoto Duniani (UNICEF),Shirika la maendeleo Canada na Tigo.

Mkuu huyo alisema kuwa mpango huo ni mpango endelevu na kwa maslahi mapana ya taifa hivyo hakuna sababu yoyote ambao inaweza kuingilia kati kwa nia ya kudhoofisha zoezi hilo.

Akizungumzia mkakati wa  Mkoa wa Singida kuhakikisha kuhakikisha wanafanya juhudi za kuandikisha watoto wote kwa kipindi cha wiki mbili zilizobaki.

Kwa upande wa Mamlaka wake Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), Emmy Hudson alisema kuwa uandikishwaji na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa ulianzishwa enzi za mkoloni.

Hata hivyo alisema kuwa kuwa kutokana na watu wengi kutokuwa na vyeti vya kuzaliwa na kujikuta wanakumbana na changamoto nyingi za kihuduma serikali Mkurugenzi iliona ni vyema kuanzisha utaaji wa vyeti hivyo katika vituo vyote vya afya na ofisi za kata.

Emmy alisema katika hatua hiyo tangu kuanzishwa kwa mpango huo tangu mwaka 2013 tayari watoto milioni tatu wameandikishwa.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!