Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Uchaguzi Mkuu: Jimbo la Ngara wagombea CCM, Chadema ‘kupasuana’
Habari za Siasa

Uchaguzi Mkuu: Jimbo la Ngara wagombea CCM, Chadema ‘kupasuana’

Philimon Charles, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Ngara
Spread the love

ZAIDI ya watia nia 30 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamejitokeza kutaka kugombea Jimbo la Ngara, Kagera kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mwaka huu. Anaripoti Danson Kaijage, Kagera … (endelea).

Alex Gashaza (CCM), ndio mbunge anayemaliza muda wake. Watia nia kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamefika watano mpaka leo tarehe 3 Julai 2020.

Kata zote 22 za jimbo hilo zinaongozwa na CCM, mbunge wa sasa (Gashaza) anapambana kutetea nafasi yake. Jimbo Ngara, mtia nia wa Chadema anasema ‘CCM ni zamu yao kuisoma namba’ kwenye jimbo hilo.

Akizungumza na MwanaHALIS Online Philimon Charles, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Ngara ambaye pia ni Mratibu wa Uchaguzi amesema, mwaka huu CCM watakabidhi kata zote 22 kwao ikiwa ni pamoja na ubunge.

Amesema, kutokana na ari ya wanachama wa Chadema kuifumua CCM kwenye jimbo hilo, watia nia zaidi ya sita wamejitokeza katika kila kata.

Alex Gashaza, Mbunge wa Ngara (CCM)

Amesisistiza kwamba, kwenye uchaguzi huu, Chadema hakitakubali kuonewa kama ilivyozoeleka akihusisha na kile kilichotokea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2018.

“Chadema ni chama kikuu cha upinzani na hatufanyi siasa za majaribio, tunafanya siasa za kuchukua dola na kupata utawala. Kwa maana hiyo, naomba kutoa taadhari kwa wasimamizi wa uchaguzi na vyombo vya dola kutoingilia mchakato na badala yake kinachotakiwa ni haki kutendeka.

“Hatutakubali kuona kilichofanyika katika uchaguzi wa serikali za mitaa kikijirudia, tuna wagombea katika kata zote 22 katika udiwani pamoja na ubunge. Tuna uhakika wa kushinda,” amesema.

Charles amesema, mwaka huu Chadema haitapokea wagombea waliokata kutoka kwenye vyama vyao kwa kuwa, waliopo na waliojitokeza wana uwezo wa kutosha.

“Tunahakikisha tunapata wagombea ambao wamekitumikia chama kwa mda mrefu, na ambao wamekifia chama pia uzoefu ndani ya chama. Pia wale walio na malengo mazuri ya kukijenga chama,” amesema Charles.

Mbunge Gashaza – anayemaliza muda wake – amesema, hatishiki na ushindani ndani ya CCM wala nje ya chama hicho.

“Ndani ya chama changu wamejitokeza watia nia kwa njia ya ubunge zaidi ya 30, kwenye kata ndo usiseme lakini mimi nipo imara na sina hofu,” amesema Gashaza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!