Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tundu Lissu kurejea Tanzania J’tatu mchana
Habari za Siasa

Tundu Lissu kurejea Tanzania J’tatu mchana

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara
Spread the love

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini Tanzania cha Chadema- Bara, Tundu Lissu amesema, atarejea nchini Tanzania Jumatatu Julai 27, 2020 saa 7.20 mchana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Lissu amesema, atarejea kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia itakayotua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Mwanasiasa huyo amesema hayo leo Jumanne tarehe 21 Julai 2020 wakati akizungumza kwa njia ya mtandao safari yake ya kurejea Tanzania kutoka nchini Ubelgiji.

Lissu amekuwa nje ya Tanzania tangu tarehe 7 Septemba, 2017 aliposhambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana akiwa nje ya makazi yake Area D jijini Dodoma.

Alifikwa na mkasa huo mchana wakati akitoka kuhudhuria mkutano wa Bunge uliokuwa ukiendelea.

Baada ya kushambuliwa, Lissu alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma kwa matibabu ya awali na usiku huo huo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

Lissu alipata matibabu hospitalini hapo hadi tarehe 6 Januari 2018 alipohamishiwa nchini Ubelgiji kwa matibabu na tayari amekwisha kueleza yeye mwenyewe amepona.

Katika mazungumzo yake leo, Lissu amerejea kuwashukuru Watanzania, Wakenya na Wabelgiji na watu mbalimbali waliojitolea kumsaidia kuhakikisha anapona akisema hatowasahau.

Lissu ni miongoni mwa wanachama saba wa Chadema waliochukua na kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa na chama hicho kugombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020.

Amesema, amekaa Ubelgiji kwa miaka miwili na nusu huku akiwashukuru majirani zake kwa kumhifadhi kwa kipindi chote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!