Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Gwajima: Tutaishinda Chadema kabla ya sadaka ya kwanza
Habari za Siasa

Gwajima: Tutaishinda Chadema kabla ya sadaka ya kwanza

Askofu Josephat Gwajima (katikati)
Spread the love

ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema yeye ni mtu pekee atakayeweza kurudisha jimbo la Kawe kwenye himaya ya Chama cha Mapinduzi (CCM) asubuhi na mapema. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Askofu Gwajima amesema hayo leo Jumanne tarehe 21 Julai 2020 wakati wa mkutano mkuu wa jimbo la Kawe, Dar es Salaam kunakofanyika kura za maoni.

Wagombea waliojitokeza ni 170 wakiwania kupitishwa na CCM kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.

Jimbo hilo kwa miaka kumi mfululizo kuanzia 2010-2020 linaongozwa na Halima Mdee wa Chadema ambaye tayari amekwisha kushinda naye kura za maoni kutetea nafasi hiyo.

Akijinadi mbele ya wajumbe, Askofu Gwajima amesema atamshinda mgombea wa Chadema mapema kabla ya sadaka ya kwanza ya ibada haijatoka.

“Nitamshinda mgombea wa Chadema asubuhi na mapema kabla sadaka ya kwanza ya ibada haijatoka na mimi ni mtu pekee nitakaye rudishia jimbo lako asubuhi na mapema, tumesha wachinjia shimoni,” amesema Askofu Gwajima.

Upigaji kura umekwisha malizika na sasa uhesabuji wa kura unaendelea.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari zaidi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!