Sunday , 3 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mpinzani wa Prof. Kitila asema mchakato haujaisha, tusubiri vikao 
Habari za Siasa

Mpinzani wa Prof. Kitila asema mchakato haujaisha, tusubiri vikao 

Mwantum Mgonja
Spread the love

MWANTUM Mgonja, aliyeshika nafasi ya pili katika kura za maoni Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam za Chama Cha Mapinduzi (CCM), anamshukuru Mungu kwa matokeo aliyoyapata na anasubiri uamuzi wa vikao vya chama. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Jana tarehe 20 Julai 2020, wajumbe wa mkutano mkuu Jimbo la Ubungo, jijini Dar es Salaam, walifanya kura za maoni za kupendekeza mgombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020.

Katika mchakato huo, Prof. Kitila Mkumbo alishinda kwa kura 172 kati ya 368 zilizopigwa huku Mgonja akishika nafasi ya pili baada ya kupata kura 73, wakati Mhandisi Burton Kihaka, akishika nafasi ya tatu akipata kura 18.

Akizungumzia matokeo hayo, Mgonja amesema anamshukuru Mungu kwa kupata matokeo hayo na kwamba anasubiri maamuzi ya mwisho ya vikao vya chama, vitakavyompitisha rasmi mgombea wa jimbo la Ubungo.

Mgonja amesema, mchakato wa jana Jumatatu sio wa mwisho, kwa kuwa bado unaendelea kwenye ngazi ya wilaya, mkoa na hata CCM taifa.

“Namshukuru Mungu sababu hiyo ndio alivyonipangia, kwenye siasa unavyoenda ukumbini usiseme lazima ni wewe. Nimeshika nafasi ya pili, nawashukuru walionipigia kura.”

“Tuache maamuzi mengine ya chama, mchakato huu ni wa awali bado unaendelea, tusubii maamuzi ya chama,” amesema Mgonja.

Prof. Kitila Mkumbo

Naye Prof. Mkumbo amesema, anasubiri hatua zinazofuata, kwa kuwa kushinda kura za maoni, sio uthibitisho wa yeye kuwa mgombea wa jimbo hilo.

“Muhimu kwamba hapa tulikuwa hatutafuti mshindi, wajumbe wa mkutano mkuu walikuwa wanatoa maoni yao kuhusu nani awe mgombea, na mimi sijashinda isipokuwa nimeweza kuongoza kura za maoni,” amesema Prof. Mkumbo

“Tumesaidia vikao vya uteuzi kupata mgombea Ubungo, tunasubiri hatua zinazofuata vikao vya uteuzi kuanzia wilaya, mkoa na hadi ngazi ya kitaifa.”

Kwa mujibu wa ratiba ya CCM, baada ya kura za maoni, tarehe 30 Julai 2020 Kamati za Siasa za Jimbo zinafanya vikao vya kuwajadili watia nia waliopendekezwa na Mkutano Mkuu wa Majimbo. Kisha kupeleka mapendekezo yake kwa Kamati za Siasa za Wilaya.

Tarehe 1 hadi 2 Agosti 2020, Kamati za Siasa za Wilaya zinaketi kujadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati za Siasa za Mikoa. Ambazo zitaketi tarehe 4 hadi 5 Agosti 2020.

Kisha, Kamati za Siasa za Mikoa kisha zitatoa mapendekezo yake kwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa (NEC) kwa ajili ya uamuzi wa mwisho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko aagiza wakurugenzi TANESCO kukemea rushwa kwenye maeneo yao

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Tunastawisha ufisadi na kuchukia matunda yake

Spread the loveBUNGE la Jamhuri linaloendelea mjini Dodoma, kwa wiki nzima limetawaliwa...

error: Content is protected !!