Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa TRA inakwama kukusanya kodi Mbagala-Mbunge
Habari za Siasa

TRA inakwama kukusanya kodi Mbagala-Mbunge

Spread the love

ISSA Mangungu, Mbunge wa Mbagala ameishauri serikali irudishe mamlaka ya kukusanya kodi ya majengo kwa halmashauri, akidai kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), inakwama kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi. Anaripoti Danson Tibason, Dodoma … (endelea).

Mangungu ametoa ushauri huo leo tarehe 9 Septemba 2019 bungeni jijini Dodoma, akisema kwamba TRA inashindwa kufikia malengo ya kukusanya kodi ya majengo hasa katika maeneo yasiyopimwa, kutokana na upungufu wa watumishi.

“Ni lini serikali itaifanya Wilaya ya Mbagala kuwa mkoa wa kikodi ili waweze kukusanya vizuri kodi katika maeneo yasiyopimwa.

Sababu yameachwa kwa asilimia kubwa na wanashindwa kufikia huko kwa sababu TRA hawana ‘man power’ ya kutosha kama hawawezi basi warudishe kwenye halmashauri zetu ili waendelee na zoezi hili,” amesema Mangungu.

Akijibu swali hilo, Dk. Ashatu Kijaji, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango amesema serikali italifanyia kazi suala hilo ili TRA iweze kukusanya kodi kwa ufanisi.

 “Hili ni jambo la kiutaratibu naomba nilichukue tutakwenda kulifanyia kazi ili tuone lini wilaya ya Mbagala inakuwa mkoa wa kikodi ili tuweze kushughulikia ukusanyaji kodi kwa ufanisi,” amejibu Dk. Kijaji.

Katika hatua nyingine, Mangungu amesema kuna changamoto ya wananchi ambao maeneo yao hayajapimwa kubambikiwa kiwango kikubwa cha kodi ya majengo, na kumuomba Dk. Kijaji kwenda katika maeneo yenye changamoto hiyo.

“Ningemuomba mheshimiwa waziri kama atakubali ombi langu la kuongozana na mimi ili akaangalie jinsi gani wananchi wanavyokadiriwa makadirio ya juu yasiyo na haki na kuwapa usumbufu mkubwa hasa wanaoishi katika maeneo yasiyopimwa,” amesema Mangungu.

Hata hivyo, Dk. Kijaji amesema hakuna mwananchi anayepewa makadirio ya juu ya kodi ya majengo kwa kuwa serikali imetangaza viwango maalumu vya kodi hiyo.

“Kuhusu wananchi kukadiriwa gharama kubwa kwa ajili ya kulipa kodi ya majengo, naomba niwaambie Watanzania kwamba dhamira njema ya serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli ya kuhakikisha wananchi hawaumizwi tena na kodi,” amesema Dk. Kijaji na kuongeza;

“Kodi  hizi tayari bunge lilishapitisha sheria sasa kila jengo ambalo ni la chini ni sh 10,000 kwa hiyo hakuna anayelipa zaidi ya 10,000 kwa kila jengo ambalo ni la chini, na kwa majengo ya ghorofa kwa kila flow ya ghorofa ni sh. 50,000 kwa hiyo hakuna makadirio yoyote ya juu.”

Aidha, Dk. Kijaji amesema kwa mwaka wa fedha wa 2017/18 TRA imefanikiwa kukusanya kodi ya majengo kiasi cha Sh. 3.77 Bilioni ikiwa ni sawa na asilimia 60 ya lengo la kukusanya zaidi ya Sh. 6 Bilioni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!