April 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Balozi Ndobho afariki dunia

Spread the love

BALOZI Paul Ndobho, aliyewahi kuwa Mbunge wa Musoma vijijini kupitia NCCR-Mageuzi, amefariki dunia katika Hospitali ya Bugando, jijini Mwanza. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 9 Septemba 2019 na Profesa Sospeter Muhongo, mbunge wa sasa wa jimbo hilo.

Taarifa ya Prof. Muhongo inaeleza kuwa, Balozi Ndobho amefariki dunia jana tarehe 8 Septemba 2019 saa 2 usiku.

“Aliyepata kuwa Mbunge wa Musoma Vijijini (NCCR-Mageuzi), Balozi Ndobho, amefariki dunia. Balozi Ndobho amekutwa na mauti jana Jumapili, 08.09.2019, saa 2 usiku akiwa kwenye matibabu kwenye Hospitali ya Bugando, jijini Mwanza,” imeeleza taarifa hiyo na kuwa taratibu za mazishi zinaendelea.

Balozi Ndobho alikuwa Mbunge wa Musoma Kaskazini mwaka 1965, na Musoma Vijijini mwaka 1995. Pia aliwahi kuwa Katibu wa Chama cha TANU, Mkoa wa Kigoma mwaka 1970.

error: Content is protected !!