November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ratiba mazishi ya Mugabe

Marehemu Robert Mugabe enzi za uhai wake

Spread the love

MWILI wa Robert Mugabe, aliyekuwa Rais Mstaafu wa Zimbabwe unatarajiwa kuwasili nchini mwake tarehe 11 Septemba 2019, ukitokea Singapore alikofariki dunia wakati anapatiwa matibabu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Ratiba hiyo imetolewa jana tarehe 8 Septemba 2019 na Wizara ya Mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa.

Taarifa ya wizara hiyo inaeleza, shughuli ya kiserikali ya kuuaga mwili wa Mugabe itafanyika Jumamosi tarehe 14 Septemba 2019 katika Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe ulioko Harare nchini humo, wakati mazishi yakitarajiwa kufanyika siku ya Jumapili tarehe 15 Septemba 2019.

Hata hivyo, taarifa hiyo haijaweka wazi eneo ambalo rais huyo mstaafu wa Zimbabwe aliyetawala kwa zaidi ya miaka 37, atazikwa.

Taarifa za Mugabe kufariki dunia zilianza kusambaa tarehe 6 Septemba 2019. Kiongozi huyo amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95. Aliiongoza nchi ya Zimbabwe kuanzia mwaka 1980 hadi mwaka 2017 aliondolewa madarakani na jeshi la nchi hiyo.

error: Content is protected !!