Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Michezo Tanzania, wapewa Uganda na Cape Verde AFCON 2019
Michezo

Tanzania, wapewa Uganda na Cape Verde AFCON 2019

Kombe la Mataifa Afrika
Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), imetoa droo ya makundi 12, kwa ajili ya michezo ya kufuzu kwa michuano ya Kombe la Mataifa Africa AFCON mwaka 2019 itakayofanyika nchini Cameroon ambaye amefuzu kama mwenyeji wa mashindano hayo akiwa kwenye kundi B, pamoja na Morocco.

Katika makundi hayo Tanzania imepangwa kundi L, ikiwa sambamba na timu za taifa ya Uganda, Cape Verde na Lesotho katika michezo inayotajalijia kuanza kupigwa Juni 5 mwaka huu, huku Tanzania akianza kucheza nyumbani dhidi ya Lesotho.

Timu itakayoongoza katika kila kundi itafuzu moja kwa moja sambamba na mwenyeji Cameroon na kufanya kuwa na jumla ya timu 13, huku timu tatu zitakazo shika nafasi ya pili nakufanikiwa kupata alama nyingi kwenye hatua ya makundi nazo zitafanikiwa kufuzu na kufanya idadi ya timu 16 zitakazoanza kuchuana Januari 2019.

Tanzania ambayo mara ya mwisho kushiriki michuano hiyo ilikuwa mwaka 1980 huwenda ikapata wakati mgumu kutoka kwa Uganda ambao pia wapo kwenye michauno hiyo inayotarajia kuanza kesho na Capeverde walishiriki michuano hiyo 2013 kutokana na kupiga hatua kubwa kwenye soka.

Makundi kamili kama ifuatavyo, kundi A: Senegal, Ikweta ya Guinea, Sudan, Sao Tome/Madagascar, kundi B ni Cameroon, Morocco, Malawi, Comoros au Mauritius, kundi C ni Mali, Gabon, Burundi, Djibouti au Sudan Kusini, kundi D ni Algeria, Togo, Benin na Gambia, kundi E ni Nigeria, Afrika Kusini, Libya na  Shelisheli na kundi F ni Ghana, Ethiopia, Sierra Leone na Kenya.

Kundi G ni DR Congo, Congo, Zimbabwe na Liberia, kundi H ni Ivory Coast, Guinea, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Rwanda, kundi I ni Burkina Faso, Angola, Botswana na Mauritania, kundi J ni Tunisia, Misri, Niger na Swaziland, kundi K ni Zambia, Msumbiji, Guinea-Bissau na Namibia na kundi L ni Cape Verde, Uganda, Tanzania na Lesotho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!