WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene amewataka wananchi kuchangamkia fursa za kimaendeleo zinazopatikana katika mkoa wa Dodoma kutokana na uwepo kwa makao makuu, anaandika Dany Tibason.
Mbali na kuwataka kuchangamkia fursa kiongozi huyo, amewataka wananchi kuacha tabia ya kubweteka na kusubiria misaada kutoka kwa wafadhili.
Alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa Benki ya DCB Commercial Bank uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa LAPF mjini Dodoma.
Simbachawene amesema ili kuondokana na umasikini ni vyema kila mtanzania kuhakikisha anafanya kazi huku wakichangamkia fursa ambazo zinatokana na taasisi za kibenki.
Kutokana na Dodoma kuwa makao maku ya nchi kuna kila sababu ya kutumia taasisi za kifedha kwa ajili ya kuomba mikopo kwa lengo la kujiendeleza kiuchumi.
“Lazima Dodoma ipewe kipaumbele ya kujiendeleza kiuchumi na mfano mzuri sasa ni kuitumia benki ya DCB abayo kwa sasa imezinduliwa rasm katika mkoa wa Dodoma kutoka na umuhimu Dodoma kuwa makao makuu.
Akizungumzia DCB aliwataka wananchi kujiunga na benki hiyo ili kuweza kufungua akaunti ili kuweza kupata mkopo kwa masharti nafuu pamoja na kutoza riba kidogo ambayo ni miatano kwa mwezi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Benki ya DCB,Edson Mkwawa amesema bnki hiyo inalenga kuwakomboa wananchi ili kuhakikisha wanapata mikopo ya riba nafuu kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.
Amesema ili wananchi waweze kuondokana na umasikini ni jambo jema wakajiunga katika vikundi pamja na kukopa mikopo kwa riba nafuu zaidi kwa lengo la kujiongezea kipata.
Leave a comment