Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali ikisema hakuna njaa, bei ya unga juu
Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali ikisema hakuna njaa, bei ya unga juu

Vyakula vya nafaka vikiwa sokoni
Spread the love

WAKATI Serikali ikijinasibu kuwa nchini hakuna njaa, bado jamii imeendelea kulalamikia upandaji wa bei ya vyakula, anaandika Dany Tibason.

Kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma wameitaka serikali kufanya jitihada za kuhakikisha bei ya vyakula kushuka bei hususani unga wa ugali pamoja na mahindi.

Naye Leah Mauza amesema kwa sasa bei ya vyakula inatishia amani kutokana na kupanda kwa bei ya vyakula huku hela ikiwa ngumu kupatikana.

Akizungumza na MwanaHALISI Online amesema kwa sasa unga wa ugali umepanda bei kutoka Sh. 2,000 kwa kila hadi kufikia Sh. 2,500.

“Kwa wiki moja iliyopita debe la mahindi lilikuwa likiuzwa kwa sh 28000 hadi 30,000 lakini kwa sasa debe la mahindi limepaa hadi kufikia kati y ash.34000 hadi 35000.

“Kwa sasa kisado cha viazi kilikuwa kikiuzwa kwa Sh. 30,00 hadi 40,00 lakini kwa sasa bei imepanda hadi kufikia kati ya 5,000 hadi 6,000 jambo ambalo ni hatari zaidi,” amesema Leah.

Naye ni mfanyabiashara wa chakula ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema wanalazimika kupandisha bei ya vyakula kutokana na hali yenyewe ilivyo.

“Hatuwezi kufanya bishara ya hasara, kila mtu anajua kuwa hali ya hewa ilikuwa mbaya sana mvua haikunyesha ya kutosha hivyo kwa sasa tunalazimika kuuza unga wa ugali kwa bei ya juu maana kwa sasa unga unauzwa kwa bei ya juu kuliko mchele,” amesema.

Hata hivyo kwa upande wa akina mama lishe wamesema biashara imekuwa mbaya kutokana na kukosekana kwa wateja na wale ambao wanapatikana wanalalamika kwa madai kuwa bei ni kubwa.

Hata hivyo mama lishe huyo amesema kwa sasa wanalazimika kupunguza kipimo cha chakula katika sahani jambo ambalo linawafanya hata wateja kulalamika.

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

error: Content is protected !!