Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sakata la Lissu: Membe amshangaa Spika Ndugai
Habari za Siasa

Sakata la Lissu: Membe amshangaa Spika Ndugai

Spread the love

BERNARD Membe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Awamu ya Nne, ameshangazwa na hatua ya Job Ndugai, Spika wa Bunge kumvua ubunge Tundu Lissu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Spika Ndugai alimvua ubunge Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki wiki iliyopita kwa madai ya utoro pia kutojaza fomu yake ya maadili.

Akizungumia uamuzi huo leo tarehe 2 Julai 2019 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Membe amesema, Spika Ndugai, Serikali na Mahakama kwa pamoja wanajua wapi alipo Lissu na sababu za kumfanya kuwepo kule alipo sasa.

Amesema, Lissu ni msomi tena mwanasheria na kwamba, bila shaka pale ataporejea tarehe 7 Septemba mwaka huu kama alivyoahidi, alifikisha suala hilo mahakamani kupinga uamuzi wa Spika Ndugai.

“Tundu Lissu kuvuliwa ubunge, mimi kama Mtanzania nilishangazwa, sasa tusubiri Lissu aje. Nina uhakika kabisa atakwenda mahakamani, kama kuna haki ataipata mahamakani,” amesema Membe.

Wakati huo huo, Membe amekemea tabia ya watu kutekwa na watu wasiojulikana, huku akiwataka viongozi wastaafu kupaza sauti zao kuukemea utamaduni huo, kwa kuwa unaleta hofu kwa wananchi.

“Niwaombe viongozi wote wa chama na serikali kulikemea jambo hili ili lisitokee, tufikiri sisi wenyewe kama watoto wetu wangetekwa ingekuwaje?

“Kwa vyovyote vile, hali hii ikiendelea wenzetu wanaowekeza kote duniani watashindwa kuwekeza nchini kwetu na wageni mbalimbali wataogopa kuja,” amesema Membe.

Mwanasiasa huyo nguli amesema, utamaduni wa kutekana ni mpya na haukuwepo hapo mwanzo.

“Suala la utekaji ni utamaduni ambao hatukuwa nao mwanzo, tunahitaji viongozi kulikemea suala hili. Viongozi wa serikali wasione aibu.

“Viongozi wa vyama vyote walikemee hili, wasilikwepe na kutuletea vitu vingine ambavyo havina msingi, viongozi wa dini zote na wastaafu wote, tusione kama shughuli zetu zimeisha. Lazima tukemee huu utamaduni mpya.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!