April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Msaidizi wa Zitto ‘aokotwa’ Kenya

Spread the love

RAPHAEL Ongangi, aliyekuwa Msaidizi wa Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo amepatikana akiwa hai asubuhi ya leo tarehe 2 Julai 2019, eneo la Mtwapa mjini Mombasa, Kenya. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Taarifa za kupatikana kwa Ongangi zimetolewa leo mchana na mke wake, Veronica Kundya akisema kwamba, mumewe amepatikana akiwa salama mjini Mombasa.

Veronica amesema, amewasiliana na mumewe kwa njia ya simu na kumhakikishia kwamba, yuko salama.

Veronica amemshukuru Mungu pamoja na watu wote waliojitokeza kupaza sauti zao, tangu Ongangi alipotekwa na watu wasiojulikana tarehe 24 Juni 2019 jijini Dar es Salaam.

“Nipo hapa leo nikiwa na furaha kubwa sana sana kuushuhudia ukuu wa Mungu. My Raphael (Ongangi) amepatikana leo Mombasa na yupo salama, sina taarifa zingine zaidi ya hiyo, ila hiyo pia inatosha sana kwangu. 

“Napenda kuwashukuru wote kwa moyo wangu wote kwa niaba ya familia yangu kwa sala na kujitoa kwenu kwa hali na mali kwenye kipindi hiki kigumu. Mimi na familia yangu tutaishi kutangaza ukuu wa Mungu

error: Content is protected !!