Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ripoti ya IMF: Serikali yajaribu kujitakasa
Habari za SiasaTangulizi

Ripoti ya IMF: Serikali yajaribu kujitakasa

Dk. Philip Mpango
Spread the love

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, amekana madai kuwa serikali imeliomba Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kutochapisha taarifa yake ya uchambuzi wa hali ya uchumi nchini kwa mwaka 2019. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Dk. Mpango ametoa kauli hiyo, siku mbili baada ya mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Zuberi Kabwe, kuituhumu serikali kuzuia IMF kuichapisha ripoti hiyo.

 Mwanasiasa huyo machachari nchini, aliahidi kuitoa ripoti hiyo baada ya kumalizika kwa sikukuu ya Pasaka. Amedai kuwa serikali imekataza ripoti hiyo kuchapishwa kwenye tovuti ya shirika hilo la kimataifa.

Akizungumza bungeni mjini Dodoma, leo 23 Aprili 2019, Dk. Mpango alisema, “serikali ya Tanzania, haijaizua IMF kuchapa ripoti hiyo.”

Amesema, kwa sasa, serikali inaendelea na mazungumzo na Mkurugenzi wa IMF, ukanda wa Afrika, Abebe Selassie, ili kuhakikisha maoni ya Serikali ya Tanzania kuhusu taarifa hiyo yanazingatiwa kabla ya kuchapishwa.

“…timu ya IMF ilikuwapo nchini kuanzia 26 Novemba hadi 7  Desemba 2018, na baada ya pale walitoa taarifa na utaratibu ni kuwa wakitoa hiyo rasimu ya taarifa, inarudi serikalini ili tuweze kuitolea maoni na wao waweze kuyazingatia kabla ya kuichapisha,” ameeleza Dk. Mpango.

Amesema, “na sisi tumepeleka maoni yetu, maoni ambayo hayajazingatiwa kwenye taarifa, na mheshimiwa spika, nilipokuwa Washngton juzi, nilizungumza na Selassie na mpaka leo saa tisa, bado tutaendeleza majadiliano kuhusu jambo hili.”

Amesema, hakuna sababu ya baadhi ya watu kuwahisha taarifa hiyo kuchapishwa, kwa kuwa muda bado upo na kwamba baada ya majadiliano ya pande zote mbili kukamilika na muafaka kupatikana, ripoti hiyo itachapishwa kwa mujibu wa sheria.

“Utaratibu ni kwamba, baada ya bodi ya wakurugenzi kuijadili hiyo taarifa, serikali inakuwa na siku 14 za kuipitia na kusema itolewe ama isitolewe,” ameeleza.

Anasema, “kwa hiyo, wasiwahishe mjadala, serikali bado inazungumza na IMF na hakuna sehemu ambayo tumezuia, ni utaratibu wa IMF yenyewe.”
Naye mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, ameitaka serikali kuruhusu IMF kuchapisha ripoti hiyo.

Kwa mujibu wa Prof. Lipumba, kitendo cha waziri wa fedha kuizuia IMF kuchapisha ripoti hiyo kwenye tovuti yake, kinaiweka Tanzania kwenye picha mbaya kuwa haina uwazi; serikali haitaki kukosolewa ama haiko tayari kurekebisha makosa au mapungufu ya sera zake.”

Alitoa kauli hiyo, kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, uliofanyika makao makuu ya chama hicho, Buguruni, jijini Dar es Salaam.

Akiwa na taarifa anayodai kuwa imezuiwa kuchapishwa, Prof. Lipumba amesema, “ni vyema taarifa hii ikachapishwa ili Bunge na wananchi wakaisoma, hata kama hawakubaliani na kilichomo. Inapokataa isichapishwe inaonekana kama kuna kitu unakificha.”

Kwa wiki kadhaa, hoja juu ya kudorora kwa uchumi wa taifa, imetawala kwenye vyombo vya habari vya ndani na vile vya kimataifa, ikiwamo mitandao ya kijamii.

Baadhi ya wakosoaji wa serikali wanasema, kuporomoka kwa uchumi wa taifa, kunatokana na serikali kushindwa kusimamia uchumi wake, hususani, sera yake ya fedha za kigeni, jambo ambalo limesababisha mfumuko wa bei.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!