Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ripoti ya CAG yaibua madudu Jeshi la Polisi, Lugumi
Habari za SiasaTangulizi

Ripoti ya CAG yaibua madudu Jeshi la Polisi, Lugumi

Mfanyabiashara Said Lugumi (mwenye tai) akiwasili katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuonana na Waziri, Kangi Lugola
Spread the love

UKAGUZI maalum wa ununuzi wa Mfumo wa Utambuzi wa Alama za Vidole (AFIS) wa Jeshi la Polisi, uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad umebaini madudu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa ripoti ya ukaguzi huo, iliyowekwa wazi kwa umma leo tarehe 10 Aprili 2019 katika tovuti rasmi ya Ofisi ya CAG imeeleza kuwa, Kampuni ya Lugumi Enterprise Limited, ilipewa zabuni bila kuwa na leseni ya biashara inayoendana na uuzaji na ufungaji wa mitambo ya udukuzi (AFIS).

Ripoti hiyo imebainisha kuwa, ununuzi wa mfumo huo haukuwepo kwenye bajeti iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na kwamba, utaratibu uliotumika kuhamisha fedha kutoka hazina kwenda Jeshi la Polisi, haukufuata utaratibu sahihi.

Vile vile, ukaguzi huo wa Prof. Assad ulibaini kwamba, vifaa vya utambuzi wa alama za vidole vyenye thamani ya  Sh. 1,736,056,030.45, havikufungwa kwenye magereza 35 yaliyoanishishwa, badala yake vifaa hivyo vilionekana kuhifadhiwa katika Ofisi ya Upelelezi ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

“Mafunzo ya wataalam 30 yaliyogharimu jumla ya Sh. 604,390,244 hayakufanyika. Zaidi, nilibaini monitor 58 aina ya dell zenye thamani ya Sh. 159,166100 zilizopelekwa kwenye kitengo cha Uchunguzi wa Kisayansi cha Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, havikuonekana wakati wa ukaguzi huu,” inaeleza sehemu ya ripoti hiyo ya CAG.

Pia, ripoti hiyo inaonesha uwepo wa tofauti ya bei ya jumla ya Sh. 556,647,610 kwa vifaa vinavyounda mfumo huo ambavyo vimetengenezwa na mtengenezaji mmoja, huku vikiwa na sifa moja na utendaji kazi unaofanana.

“Katika ukaguzi wangu wa mkataba baina ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Mzabuni Lugumi Enterprises Limited, nilibaini kuwa mahitaji ya kitaalamu kutoka idara ta mtumiaji wa mfumo hayakuzingatiwa wakati wa kutathimini na kutoa zabuni,” inaeleza sehemu ya ripoti hiyo.

Kampuni ya Lugumi Enterprise iliingia mkataba wa Sh. 37 bilioni na Jeshi la Polisi wa kufunga mashine za kielektroniki za kuchukua alama za vidole katika vituo vya jeshi hilo.

Katika hatua nyingine, Ripoti hiyo imeonesha matokeo ya ukaguzi maalum wa ununuzi wa sare za polisi uliofanywa na Jeshi la Polisi, ikieleza kuwa, Jeshi la Polisi lilipa jumla ya Sh. 16,660,000,000 bila ya kuwa na ushahidi wa uagizaji na upokeaji wa sare hizo kwa Boharia Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!