April 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mke wa Robert Kisena kuburuzwa kizimbani

Nyundo ya Hakimu

Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru inatarajia kumburuza kortini Florencia Mashauri ambaye ni mke wa Robart Kisena, Mkurugenzi wa Kampuni ya Usafisirishaji ya UDART. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa Habari, Kassin Ephrem, Kaimu Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Takukuru amesema Taasisi hiyo inampandisha kizimbani Florencia ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Zenon Oil and Gas  Limited kwa tuhuma za kuhujumu uchumi na utakatishaji fedha.

Amesema kuwa mshitakiwa anakabiliwa na tuhumu ya wizi, kukiuka sheria ya mafuta na utakatishaji wa fedha. Pia anadaiwa kutakatisha kiasi cha Sh. 1.2 bilioni na kuitia hasara ya Sh. 1.2 bilioni kwa kuuza mafuta hewa

Florencia na mume wake Kisena naye ameunganishwa kwenye shauri hilo watakalofunguliwa.

MwanaHALISI Online itaendelea kukujulisha kinachoendelea katika shauri hili.

error: Content is protected !!