CHAMA cha Wananchi (CUF), upande unaongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba kimepata pigo kubwa baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kupiga marufuku bodi yake kujihusisha na shughuli zozote za chama hicho mpaka shauri la msingi litakapomalizika, anaandika Hamisi Mguta.
Profesa Lipumba ambaye anatambuliwa na msajili wa vyama siasa nchini analumbana na Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Shariff Hammad hatua ambayo imesababisha pande hizo mbili kufikishana mahakamani ili kutafuta haki.
Awali, mahakama hiyo iliyatupilia mbali maombi ya Wakili Mashaka Ngole (anayemwakilisha Lipumba) aliyokuwa anaomba Jaji asisome maamuzi hayo kwa madai kuwa Lipumba anakusudia kukata rufaa juu ya maamuzi ya Jaji kukataa kujitoa kusikiliza mashauri ya CUF.
Mahakama Kuu imesema, hakuna hoja za kisheria zinazoizuia kuacha kuendelea na shughuli ilizozipanga.
Leave a comment