Saturday , 3 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge akataliwa kusajili shule
Habari za Siasa

Mbunge akataliwa kusajili shule

Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu
Spread the love

MBUNGE wa jimbo la Itilima, Njalu Silanga (CCM) amekataliwa kupewa usajili wa shule  ya msingi Njalu iliyopo wilayani Itilima Mkoani Simiyu kwa sababu ya kutokidhi vigezo, anaandika Mwandishi wetu.

Usajili wa shule hiyo iliyojengwa na wananchi kwa kushirikiana na Mbunge Njalu Silanga wa jimbo la Itilima (CCM) umekataliwa na Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako.

Profesa Ndalichako amesema shule hiyo haijakidhi vigezo vya usajili hivyo amekataa ombi la mbunge huyo kuisajili na kuagiza upungufu uliopo urekebishwe kwanza kabla ya wizara kuisajili shule hiyo ya umma.

Miongoni mwa upungufu huo ni kuwa na vyumba vitano pekee vya madarasa kati ya vinane vinavyohitajika.

Mengine ni matundu ya vyoo, ambayo kati ya 10 yanayohitajika, yapo matano pekee, huku ikiwa na chumba kimoja cha ofisi ya walimu.

Hata hivyo, Profesa Ndalichako amesema wizara itatoa mifuko 100 ya saruji kusaidia kuondoa upungufu uliopo.

“Tumeona kuna upungufu hatutaweza kutoa kibali cha kuisajili, badala yake mkamilishe yanayohitajika kwa utaratibu wa kisheria wa kufungua shule. Niwahakikishie kuwa, Wizara ya Elimu hatuna urasimu ni lazima tuwe makini kwa kusimamia vigezo hivyo,” amesema Profesa Ndalichako.

Amesema licha ya kuwapo kwa mahitaji ya shule katika eneo hilo ambalo lina wanafunzi wapatao 633, ni lazima kuzingatia vigezo ambavyo vitakaguliwa na wataalamu kutoka idara ya udhibiti ubora wa elimu na ofisi ya ofisa elimu wilaya.

Silanga alimwomba Waziri Ndalichako kuwapatia usajili wakati wakiendelea kushughulikia upungufu uliojitokeza kwa kipindi cha muda mfupi kabla ya shule kufunguliwa Januari 8 mwakani ombi ambalo hata hivyo, lilikataliwa.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!