March 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sumatra yatangaza vita kwa wamiliki mabasi

Kituo cha mabasi Ubungo, Dar es Salaam.

Spread the love

BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), limetoa wito kwa abiria waendao mikoani kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka, kutokata tiketi kiholela na kuhakikisha imeandikwa jina la basi husika pamoja na kuonyesha kiasi cha nauli waliyolipa, anaandika Angel Willium.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nchi Kavu na Majini, Oscar Kikoyo amesema kutokana na wingi wa abiria kipindi cha mwisho wa mwaka, baadhi ya watoa huduma wasiokuwa waaminifu huwaibia wasafiri kwa kuongeza nauli.

“Baadhi ya abiria wanakubali kienyeji, analipa Sh. 70,000 anapewa tiketi ya Sh. 50,000 tunawasihi sana abiria kuwa makini na kutoa taarifa, kushirikiana na mamlaka husika iwapo vitendo vya namna hiyo vitajitokeza” amesema Kikoyo.

Kikoyo amesema abiria wanatakiwa kutonunua tiketi za safari, kutoka kwa wapiga debe au vishoka katika eneo la kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam na vituo vingine nchini kote.

Aidha, Kikoyo amesema kutokana na mahitaji makubwa ya usafiri, baadhi ya abiria hukubali kulipa fedha zaidi ili wasafiri na Baraza linachukua fursa hii kuwakumbusha Wamiliki wa Mabasi yaendayo Mikoani (TABOA), kwamba watafutiwa masharti ya leseni zao na kutoa nauli zilizoidhinishwa na SUMATRA.

Kipindi cha mwisho wa mwaka, Watanzania wengi wanasafiri kwenda mikoani kwa ajili ya kuungana na jamaa zao kusherekea sikukuu ya krismass na mwaka mpya.

error: Content is protected !!